Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Umasikini sio sifa, umasikini sio jambo la kujivunia.
Siku zote tunapaswa kuwaongoza wananchi wetu ili wauchukie umasikini na wapende kuwa na maendeleo.
Nimesikitishwa sana na maneno aliyosema Dr Hamis Kigwangala kule twitter kupinga vigezo vilivyowekwa na kampuni yetu ya TRC kukataza watu kupanda na wanyama pamoja na vitu ambavyo vinaweza kusababisha mradi ukose utunzaji mzuri na hatimaye kuharibiwa kutokana na kukosa tu umakini.
Nipende kuwapa moyo TRC. Msikate tamaa, endeleeni na misimamo yenu maana misimamo yenu ndiyo itakayohakikisha mradi ule unakuwa na ubora wake kwa muda mrefu. Tukianza kuruhusu mambo ya ajabu katika mradi huu, mradi huu utaharibiwa mapema sana na hawa wanasiasa wajinga watakuja kuwasema kuwa ham kuchukua hatua stahiki hadi kupelekea mradi kuharibika.
Nirudi kwa Serikali yangu.
Hivi inakuwaje mnaanzisha safari ya kutoka Dar- Morogoro wakati morogoro ham kufanya maandalizi ya uhakika kujenga kituo cha kisasa cha taxi, dalalala pamoja na pikipiki bila kusahau barabara nzuri za uhakika kutoka kituo cha kushusha abiria cha Morogoro hadi barabara kuu?
Hivi mnadhani watanzania wanajiskiaje mkipeleka wasanii Korea kwa kodi zao huku mkishindwa kutengeneza barabara ya umbali mfupi tu hadi kufanya abiria anatoka kwenye usafiri mzuri alafu anaingia kula mavumbi?
Hivi mlishindwa hata kutengeneza kituo kidogo tu cha daladala na Taxi/ Bajaji na kuweka sehemu nzuri ya wafanyabiashara kufanya biashara kwa staha na usafi hadi mnafanya mama ntilie wanabeba vyakula na kuweka chini kwenye stand ya mradi uliogharimu matrilioni ya Pesa??
Hivi kusema kweli huko Serikalini hakuna watu wenye akili timamu wanaoweza kuamua kufanya vitu kwa viwango na ubora hadi tunakuwa watu wa hovyo kiasi hiki?
Mnasikitisha sana!
Pia soma:Mabegi ya 'shangazi kaja' marufuku kwenye kwenye treni ya SGR