Treni ya SGR, Tukiamua kufanya Vitu vya Kisasa tuvifanye kwenye ukisasa wake

Nirudi kwa Serikali yangu.
Hivi inakuwaje mnaanzisha safari ya kutoka Dar- Morogoro wakati morogoro ham kufanya maandalizi ya uhakika kujenga kituo cha kisasa cha taxi, dalalala pamoja na pikipiki bila kusahau barabara nzuri za uhakika kutoka kituo cha kushusha abiria cha Morogoro hadi barabara kuu?
Ndani ya ccm unapigia mbuzi gita
 
Vile vile kituo cha SOGA Barabara yake inayotokea Kongowe ni mbovu kupita kiasi, Maana kituo hicho kingehudumia wakazi wote wa kibaha, Bagamoyo hadi Mbezi
 
Nirudi kwa Serikali yangu.
Hivi inakuwaje mnaanzisha safari ya kutoka Dar- Morogoro wakati morogoro ham kufanya maandalizi ya uhakika kujenga kituo cha kisasa cha taxi, dalalala pamoja na pikipiki bila kusahau barabara nzuri za uhakika kutoka kituo cha kushusha abiria cha Morogoro hadi barabara kuu?

Hivi mnadhani watanzania wanajiskiaje mkipeleka wasanii Korea kwa kodi zao huku mkishindwa kutengeneza barabara ya umbali mfupi tu hadi kufanya abiria anatoka kwenye usafiri mzuri alafu anaingia kula mavumbi?
We have a failed government
Inatumia matatizo ya wananchi kama fursa
 
Vile vile kituo cha SOGA Barabara yake inayotokea Kongowe ni mbovu kupita kiasi, Maana kituo hicho kingehudumia wakazi wote wa kibaha, Bagamoyo hadi Mbezi
Nashindwa kuelewa hii Serikali yetu ina vipaumbele gani? How comes mradi kama huu unakosa kupewa priority alafu wanapewa priority wasanii kupelekwa Korea?
 
Nimesikitishwa sana na maneno aliyosema Dr Hamis Kigwangala kule twitter kupinga vigezo vilivyowekwa na kampuni yetu ya TRC kukataza watu kupanda na wanyama pamoja na vitu ambavyo vinaweza kusababisha mradi ukose utunzaji mzuri na hatimaye kuharibiwa kutokana na kukosa tu umakini.
Huyu Kigwangala mbona hakutoa ushauri kama huu kwenye bombardier?
 
Sema kuna raha yake sehemu inapokuwa na utaratibu unaofuatwa. Nawaza pale Kariakoo pangekuwa pamepangiliwa vizuri kusingekuwa na msongamano vile. Serikali ikijaribu kuwaondoa wanaopanga bidhaa barabarani tunaaandamana tukidai wanyonge tunaonewa.

Pia kuhusu aina za mifuko wangetoa muongozo mmbadala wake ni upi wasiishie tu kupiga marufuku.

Sote tunatafuta pesa, tusitumie "unyonge" wetu kuharibu taratibu za mtoa huduma as long as zinaleta matokeo chanya.
 
Kweli kabisa! Ustaarabu ndo kipimo kizuri cha utu wetu na heshima yetu kama binadamu!

Ni lazima tuanze kuchukua hatua saivi ili kuwastaarabisha watu wetu wajifunze kufanya vitu kiustaarabu!
 
Back
Top Bottom