Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Rais Samia akiwasalimia wananchi katika uzinduzi wa treni Agosti 1, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amezindua rasmi huduma za usafiri wa reli ya kisasa (SGR), treni iliyokuwa imebeba wageni walioshiriki uzinduzi huo wakiwamo mabalozi na viongozi mbalimbali wa kiserikali kutokea mkoani Dodoma, imepata tena hitilafu karibu na Stesheni ya Morogoro kwa zaidi saa moja sasa.
Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme
Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:"Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."
Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."
Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.
Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC) zinaendelea.
Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku mbili baada shirika hilo kuomba radhi kwa treni yake iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete mkoani Morogoro juzi tarehe 30 Julai 2024.
Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete
“Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system),” amesema.
Mwananchi