Treni ya SGR yazimika tena Morogoro!
View attachment 3059049
Rais Samia akiwasalimia wananchi katika uzinduzi wa treni Agosti 1, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amezindua rasmi huduma za usafiri wa reli ya kisasa (SGR), treni iliyokuwa imebeba wageni walioshiriki uzinduzi huo wakiwamo mabalozi na viongozi mbalimbali wa kiserikali kutokea mkoani Dodoma, imepata tena hitilafu karibu na Stesheni ya Morogoro kwa zaidi saa moja sasa.

Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:"Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."

Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.

Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC) zinaendelea.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku mbili baada shirika hilo kuomba radhi kwa treni yake iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete mkoani Morogoro juzi tarehe 30 Julai 2024.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

“Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system),” amesema.

Mwananchi
View attachment 3059048
Precautions: Unaposafiri hakikisha una mikate,maji na juisi za safarini.
Over!!!
 
Hawa Popo na ngedere inabidi washughulikiwe haraka sana wanaweza kusababisha maafa hivi hivi.
 
Ila mwanzo mgumu acha tuwe na subra
Ndo inakufa hivyoo, we kama unataka kupanda panda sasa hivi ikiwa mpya mpya..

Ukipita mwaka inapauka kama vilivyopauka viti vya mwendokasi, milango ya mwendokasi ikiwa inafunguka utadhani vyuma vinasuguana inapiga kelele kinoma.
Na huko ndiko hii treni nayo itafika.

So enjoy before it's too late.
 
Yaani kaka angu usemayo yawez akua saihi
Naigopa sasa hyo SGR maana miye toka imeanza ndo napanda hyoo..na nilisema Mabasi tena baba jeni byebye..hapa niko Dar nataka nirudi Dom naanza kupata hofu miye
Ni sahihi kabisa tunatembea na hofu muhimu kuomba dua tu, maana kiuhalisia kuokoa muda na gharama rafiki treni ni bora zaidi. Kibongo bongo ndege wanaona ni anasa.
 
kitu chochote kipya takes time to be perfect, hii ni train ya kwanza Africa mashariki na kati ya umeme yenye urefu huu; so its not an easy task mpaka ikaja kukaa sawa
Kweli tena na hatua tuliofikia sio haba kwakweli!.. wanaopondea ni chuki tu na roho mbaya zimewajaa[emoji849][emoji849][emoji21]
 
WEKA WI-FI, WEKA WI-FI, HUU SIO MDA TENA WA KUWAZA KUISHIWA NA DATA, ROUTER NI BEI NDOGO TU!

⚫KWENYE BISASHARA YAKO WEKA WI-FI

⚫KWENYE SHULE WEKA WI-FI

⚫KANISANI WEKA WI-FI

⚫KAZINI WEKA WI-FI
⚫KWENYE KAMPUNI WEKA WI-FI

⚫NYUMBANI KWAKO WEWE NA FAMILIA YAKO WEKA WI-FI

⚫CHUONI WEKA WI-FI

⚫UNA SECURITY CAMERA FUNGA WI-FI

⚫SEHEM ZINGINE AMBAZO SIJAZITAJA WEKA WI-FI

TUMIA DATA UNLIMITED, YANI BILA KUWAZA KUA GB ZITAISHA?

NJOO NIKUPE ROUTER ZENYE UWEZO MKUBWA TECNOLOJIA YA 5G SPEED HADI 200mbps, NA UNAWEZA KULIPA KIDOGO KIDOGO !

MKOA WOWOTE ULIPO HUDUMA INAKUFIKIA NDANI YA MDA MFUPI

GHARAMA NI NAFUU SANA, ( pia laini pekeyake bila router nakuwezeshea bando unlimited kwa bei poa )
NICHEKI: 0717700921
 
Back
Top Bottom