Treni ya SGR yazimika tena Morogoro!
kitu chochote kipya takes time to be perfect, hii ni train ya kwanza Africa mashariki na kati ya umeme yenye urefu huu; so its not an easy task mpaka ikaja kukaa sawa
Ni excuse tu hakuna kitu hapo
Msijidanganye eti ya kwanza East Africa sijui mwanzo mgumu.
Ukisikia kuuziwa mbuzi kwenye gunia ndio hii
Kama nchi rushwa inatutafuna sana…

Hakuna mradi hapo
Tunashindwa umeme wa majumbani tutaweza hili kweli?

Tusiwadanganye walipa kodi tafadhalini.
 
Kitu hakina 10days unataka uone ukamilifu wake, hata binadamu wa kwanza hakua mkamilifu ilichukua muda kugundua anahitaji msaidizi, tuachane na hayo maneno, logically huwezi fikiria hiyo treni itaanza bila misukosuko ukizingatia ni mradi mkubwa na wa kwanza kwa mazingira haya, haiitaji akili ya darasa la nne kuelewa hili.
 
View attachment 3059049
Rais Samia akiwasalimia wananchi katika uzinduzi wa treni Agosti 1, 2024

Rais Samia Suluhu Hassan leo Alhamisi amezindua rasmi huduma za usafiri wa reli ya kisasa (SGR), treni iliyokuwa imebeba wageni walioshiriki uzinduzi huo wakiwamo mabalozi na viongozi mbalimbali wa kiserikali kutokea mkoani Dodoma, imepata tena hitilafu karibu na Stesheni ya Morogoro kwa zaidi saa moja sasa.

Pia soma: Morogoro: Treni ya SGR (Dar-Dodoma) yakwama Kidete Kilosa kwa zaidi ya saa 4, sababu Hitilafu ya Umeme

Mmoja wa abiria aliyemo kwenye treni hiyo amesema:"Tumetoka vizuri tu Dodoma lakini tulipofika katikati ya Mkata na Moro stesheni ikiwa kama saa 4:33 usiku ikasimama ghafla hadi na kuzima kabisa, hadi sasa saa 5:33 usiku bado tupo hapa."

Mmoja wa wahariri, Peter Nyanje katika ukurasa wake wa Instagram ameandika:"Ni saa tano usiku tulitoka Dodoma kwenye uzinduzi wa SGR. Wakati tunakaribia station ya Morogoro treni imesimama ghafla njiani, air conditions zimezima, milango haifunguki. Tumekwama hapa sasa ni zaidi ya nusu saa. Tupo takribani watu 1,000 humu ndani."

Hata hivyo, ilipofika saa 5:35 usiku, treni hiyo ilianza safari.

Juhudi za kuupata uongozi wa Shikika la Reli Tanzania (TRC) zinaendelea.

Hayo yanajiri ikiwa zimepita siku mbili baada shirika hilo kuomba radhi kwa treni yake iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma kusimama kwa muda wa saa mbili kati ya stesheni ya Kilosa na Kidete mkoani Morogoro juzi tarehe 30 Julai 2024.

Pia soma: TRC yatolea ufanunuzi kuzimika kwa treni ya SGR Julai 30, 2024 katikati ya Stesheni ya Kilosa na Kidete

“Taarifa za awali zinaonesha kuwa hitilafu za aina hiyo husababishwa na wanyama (ngedere) au ndege (bundi) wanapogusa nyaya za umeme zilizotandazwa juu ya reli (overhead catenary system),” amesema.

Mwananchi
View attachment 3059048
Acha kulia lia ukafikiri duniani kuna malaika kwamba hawakosei. Trial and error ni kawaida sana kwenye project kubwa kama hizo.
 
Sio muda wa Kukejeli Mradi...tuwe na Uzalendo kama 🇹🇿 🇹🇿
Yawezekana Mazingira ya nchi yetu yakawa ni changamoto katika Kutekeleza mradi.. huwezi kufananisha Mazingira ya Tanzania ambapo kuna Misitu / Wanyama kama Ujerumani/ UK kwa mfano..
Hapa Nashauri Wasomi wa Vtuo Vikuu Animal Scientists; Ecologists kutoka vyuo vya SUA; udsm washirikishwe ni jinsi gani Wanaweza Kuzuia Hawa Wanyama kuletA Uaribifu kwenye Huo Mradi
Tuwe na Constructive ideas kuliko kuanzA kutoa Kejeli kuonesha kila kitu kinachofanyika basi hakina Manufaa..
Au kutaka Watu watumbuliwe..
Tupende kuwekeza kwenye Uchunguzi ( Investigation) na kuja na Ufumbuzi wa Matatizo yetu
 
Ni excuse tu hakuna kitu hapo
Msijidanganye eti ya kwanza East Africa sijui mwanzo mgumu.
Ukisikia kuuziwa mbuzi kwenye gunia ndio hii
Kama nchi rushwa inatutafuna sana…

Hakuna mradi hapo
Tunashindwa umeme wa majumbani tutaweza hili kweli?

Tusiwadanganye walipa kodi tafadhalini.
Jana France bullet train imekwama station na kuzuia abiria 8000 wasisafiri.
Je hilo unalizungumziaje?
Nao FRANCE ni wapigaji wamejipiga katika miradi!?
TUSIPENDE kua na inferiority complex na negative mindset kila wakati.
Muda mwingine tufikirie in positive way kama nguvu kazi ya taifa hili.
Badala ya kuwazia mawazo asi toeni fikra za kuboresha mifumo iende sawia.Hivyo ndivyo wenzenu hufanya ndio maana wanatuzidi kimaendeleo.
 
Asante sana Mkuu, nilisom quote yake nikaona hata nikimjibu nitakua napoteza muda, nafurahi umeweza kumuelewesha
Watu weusi kiujumla tumekua ni Watu wa kujisimanga na kuwazia mawazo asi kila kukicha.
Ndio maana tumedumaa kifikra.
 
Sio muda wa Kukejeli Mradi...tuwe na Uzalendo kama 🇹🇿 🇹🇿
Yawezekana Mazingira ya nchi yetu yakawa ni changamoto katika Kutekeleza mradi.. huwezi kufananisha Mazingira ya Tanzania ambapo kuna Misitu / Wanyama kama Ujerumani/ UK kwa mfano..
Hapa Nashauri Wasomi wa Vtuo Vikuu Animal Scientists; Ecologists kutoka vyuo vya SUA; udsm washirikishwe ni jinsi gani Wanaweza Kuzuia Hawa Wanyama kuletA Uaribifu kwenye Huo Mradi
Tuwe na Constructive ideas kuliko kuanzA kutoa Kejeli kuonesha kila kitu kinachofanyika basi hakina Manufaa..
Au kutaka Watu watumbuliwe..
Tupende kuwekeza kwenye Uchunguzi ( Investigation) na kuja na Ufumbuzi wa Matatizo yetu
Bora umeongea mkuu.
Yani ukisikiliza watanzania unaweza ukaishiwa nguvu,Yani ni Watu wa kuchukulia kila kitu hakiwezekani.
Negative energy kibaaaooo.
 
Ni excuse tu hakuna kitu hapo
Msijidanganye eti ya kwanza East Africa sijui mwanzo mgumu.
Ukisikia kuuziwa mbuzi kwenye gunia ndio hii
Kama nchi rushwa inatutafuna sana…

Hakuna mradi hapo
Tunashindwa umeme wa majumbani tutaweza hili kweli?

Tusiwadanganye walipa kodi tafadhalini.
Nchi hii kila mradi wakiuanzisha utasikia ni wa kwanza EA,au duniani ni ya pili 😄
Wana mbwembwe hawa

Ova
 
Watu weusi kiujumla tumekua ni Watu wa kujisimanga na kuwazia mawazo asi kila kukicha.
Ndio maana tumedumaa kifikra.
Kujisimanga au mnaambiwa ukweli.....udart tu mpaka leo mna kata mauno tu mnacheza komasava

Ova
 
Kujisimanga au mnaambiwa ukweli.....udart tu mpaka leo mna kata mauno tu mnacheza komasava

Ova
Umeelewa ninalenga nini mkuu!?
Soma kwa uelewa kesha urejee maana HUJAELEWA.
 
Tutembee kwa miguu tusipande mabasi yao.
HAWA WENYE MABASI HUMILIKI NGUVU KALI SANA ZA GIZA TRUST ME OR NOT, UNAWEZA KUTUPWA TUNGURI HAPO MOROGORO IKALETA KERO YA KIHISTORIA, NAKUMBUKA YULE BIBI WA MTWARA ALIYEIZUIA GESI MPAKA AKAOMBWA DADEKI WACHAWI, MBWA KABISA!
 
kitu chochote kipya takes time to be perfect, hii ni train ya kwanza Africa mashariki na kati ya umeme yenye urefu huu; so its not an easy task mpaka ikaja kukaa sawa
Ile back generator Iko wapi?
 
Back
Top Bottom