13 November 2022
Songwe, Tanzania
AJALI SONGWE, GARI LAGONGA TRENI LA MIZIGO, ABIRIA WANUSURIKA KIFO..
Abiria kadhaa wamenusurika kifo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria, lenye namba za usajili T388 DUS kuligonga treni la mizigo katika makutano ya Barabara Kuu ya Tanzania na Zambia (Tanzam) katika eneo la Songwe mkoani Songwe, tukio lililotokea jioni ya Novemba 13, 2022. Picha za video kutoka eneo la tukio, zinalionesha treni ya mizigo ikiwa imepinduka baadhi ya mabehewa na kufunga barabara hiyo
Source : Global TV Online