Trial by Jury vs Bench Trial.

Trial by Jury vs Bench Trial.

pinno

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,213
Reaction score
1,229
Hodiiii Wanasheria na wadau wengine washeria.

Katika kusoma soma kwangu na kuperuzi ishu za kisheria na mifumo ya kimahakama, nikagundua kuwa kuna mifumo hii miwili, Trial by jury na Bench Trial.

Naomba kwa mdau anaeifaham vizur, aweze kunielekeza, naman ambavyo kila mfumo unafanya kazi, na upi ni mzuri na hapa kwetu Tz tunatumia mfumo gani??

Nimeona kwenye baadhi ya TV series za US zinazohusu sheria sheria (mf. Justice ya mwaka 2006) nikagundua kule wanatumia Trial by jury. na nimeipenda hii system, nataka jua mapungufu yake na mazuri yake kwa kulinganisha na bench trial. na hapa kwetu tunatumia ipi na kwa nini???.

Thanks.
 
Jury trial (system) mimi naiona ndo bora zaidi.

Ni bora kwa sababu hatima yako inaamuliwa na peers wako kwenye jamii ambao wanaweza wasiwe hata na utaalamu wa sheria lakini ni watu wenye sense of fairness.

Kuwa mtaalamu wa sheria hakumfanyi mtu awe na sense of fairness na ndo maana kwa nchi kama Marekani mtu hahitaji kuwa na shahada ya sheria kuwa jaji wa US Supreme Court.

Kwenye jury panel kunakuwa na watu kuanzia 6 hadi 12 (hii inategemea na sehemu lakini). Hao ndo waamuzi wa hatma yako - una hatia ama huna hatia. Hao watu wanakuwa na backgrounds mbalimbali - kunaweza kukawa na housewives, mafundi bomba, maprofesa, wabeba zege, na kadhalika.

Kabla ya kufikia uamuzi, huwa wana deliberate kwanza na kama wana swali au maswali yoyote yale basi hurudi kwa jaji na kuuliza ili kupewa ufafanuzi.

Ni vigumu pia kuwarubuni kwa hongo kwa sababu mara nyingi huwa wanakuwa sequestered ili wasije kuathiriwa na publicity ya kesi husika.

Lakini hata jurors nao wakati mwingine hukosea, which speaks to the fact that there is no perfect justice system anywhere in the world.

Kwa sababu nao ni watu, wakati mwingine mambo ya pre-trial publicity, preconceived notions, personal biases, na kadhalika huathiri maamuzi yao. Mfano mzuri ni kesi ya O.J. Simpson ambapo jamaa alipatikana hana hatia katika double murder trial yake licha ya kuwepo na mlima wa ushahidi dhidi yake (dna, past spousal abuse history) na yeye kukosa airtight alibi.

Ukiangalia demographic ya jury iliyomwachia, pamoja na historia ya LAPD na tukio la kupigwa Rodney King na aftermath yake, basi ni rahisi sana kuhitimisha kuwa hayo mambo yalichangia kwa kiasi kikubwa sana katika uamuzi uliofikiwa na hao jury members.

Sasa kesi zinazoendeshwa na jaji mmoja au wawili halafu hao hao ndo watoa uamuzi na hukumu, ni rahisi kuwarubuni kwa hongo.
 
Thanks Mkuu, umenitoa porini.
NI kwa sababu am not from law proffesion ila nilivutiwa tu na hii kitu , ( the only thing najua kuhusu law ni law of contract etc etc nilizo soma ktk course ya business law semister moja.)

So hapa Tz hatutumii mfumo huo wa jury? , na unadhan ni nini kinaweza zuia sisi kushindwa kutumia huo? sababu naona hata kama nao una mapungufu lakin kidogo kwenye kipengele cha kuhonga watu hapo ndo ishu! kwa nchi kama hii ambayo rushwa imejaaa sana, nadhan tuwngeweza kuisolve kwa njia hii,

Au hata kama kuna uwezekano wa kuchanganya system hizi mbili, is it possible??
 
Back
Top Bottom