Nilishtuka sana leo asubuhi niliposikia habari za msiba wa Halima! Pascal Mayalla pole kwa huu msiba kutokana na hayo uliyoyasimulia hapa!
Nakumbuka nilimuona mara ya kwanza pale studio za RTD (wakati huo), 1995, nilienda kupeleka tangazo la kupotelewa na ndugu yangu! Alikuwa wameketi ofisini na Idd Rashid Mchatta (R.I.P. waliitana shemeji), nilipowaelezea tatizo lililonipeleka. Kwa kweli walinisikitikia sana na pia kunisaidia kutoa tangazo lile!
Lakini baada ya miaka kama 6, nilifahamiana na mzazi mwenzie (Baba Yekini), ambaye baadae kwenye 2005 au 2006 miezi michache kabla hajapata stroke tulikuwa namkakati wa kuanzisha NGO tukiwa wanne (Baba Yekini, Mimi, Halima na mtangazaji mwingine wa kike wa RTD, sikumbuki jina lake).
Bahati mbaya sana Halima akapata stroke, hivyo project yetu ikafa, maana yeye ndiye alikuwa muhusika mkuu! Niungane na wale wanaomfahamu/waliomfahamu kukumbuka umahiri wake kutangaza mpira na vipindi vingine vya redio. Halafu nakumbuka Halima alipata stroke kipindi kama hiki (December) na amefariki December!
Sijui alizaliwa na kuolewa December? Just thinking loudly!
Nimefahamishwa kuwa msiba upo Mbezi Beach kwa dada yake (Sina uhakika kama ni Da Mwajuma) karibu na flats za BOT. Mazishi ni kesho saa kumi jioni kwenye makaburi ya mamwinyi Msasani! Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake Lihimidiwe! Amen.