Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!

Halima Mchuka,ni miongoni mwa Watangazaji walionivutia sana.RIP
Kumbe ndio maana nilikuwa nakuona Kanisani Msimbazi,Siku hizo nikiwa nasoma shule ya msingi Na sekondari.Nilikuwa nafurahi kukuona.Ulikuwa unakaa karibu Na Priva Mtema?

kwa hiyo mitaa ya kina HALIMA kama alikua anakaa hapo ni wazi ndio maeneo ya marehemu Privatus Mtemanyenje ambae alikua katibu mkuu wa simba sc!
 
kumbe alikua mtu fresh basi
 

Huyu Ng'wanakilala ndio babake yule kijana FUMBUKA NG'WANAKILALA mhariri wa wa moja kati ya magazeti yanayomilikiwa na mzee mengi au ni kakake?
 
Baba yake ila tu Baba kajizaa...Jamaa ni kichwa sana...

Yah kama kweli yule mtoto wa nkwabi ng'wanakilala kweli nakubali mzee kajizaa,dogo simjui sawasawa kwa maana ya elimu yake na nini lakini ukisoma jinsi anavyoandika kwa sisi wasomaji wa magazeti yote unajua kweli hili ni jembe!
 
poleni sana Familia ya Halima Mchuka. Nilisoma naye Ashira Secondary miaka hiyo ya 80. alikuwa binti mdogo kuliko
wote darasani kwake na alipenda sana michezo hasa Riadha. Mwalimu wa Michezo A. Kisonga alimpenda sana kwa
weledi wake katika michezo. Nilimuacha shule ndipo nilipomsikia akitangaza michezo RTD. Mungu amlaze Pema Peponi.
Pole sana Asha Mchuka wa Mabibo.
 
Final Update

HALIMA M. MCHUKA (18 Mar.1967- 29 Dec. 2011)​

Familia ya Mchuka wa Dar es Salaam, pamoja na ndugu wote walioko Miono na Kibindu-Bagamoyo, wanatoa shukrani za dhati kwa wote mlioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kipindi kigumu cha msiba wa mpendwa wao, Halima Mohamed Mchuka uliotokea tarehe 29/12/2011 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuzikwa tarehe 30/12/2011 katika makaburi ya Msasani Dar es Salaam.

Shukrani za pekee ziwaendee, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt.Emanuel Nchimbi, Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Mhe. Sofia Simba, Naibu Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,Mhe. Dkt. Fenella Mukangara, Waheshimiwa wabunge wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam, IGP, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mstahiki Meya wa Ilala.

Shukrani nyingine ziwaendee viongozi na wafanyakazi wa TBC wakiongozwa na M/Kiti wa Bodi ya TBC, Wilfred Nyachia na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana, wafanyakazi wastaafu wa RTD, wafanyakazi wa kampuni ya Ndege Tanzania, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Dar Group na Muhimbili, viongozi wa vyama vya michezo, waandishi wa habari na watangazaji wa vyombo mbalimbali vya habari, Uongozi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, BAMITA, majirani wa Karakata, Msasani, Mabibo na Mbezi, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia ya MCHUKA wa ndani na nje ya nchi. Tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati kwa kutufariji kufuatia kifo cha HALIMA MCHUKA.

Arobaini ya Marehemu itafanyika Miono Bagamoyo siku ya Ijumaa Tarehe 3/02/2012 kuanzia saa 11:00 jioni na Hitma itasomwa Jumamosi ya Tarehe 04/02/2012 saa 3 :00 asubuhi.Nyote mnakaribishwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na wanafamilia moja kwa moja au kupitia simu namba 0713477790 au 0784737253.Karibuni.

INNA LILLAH WAINNA ILAYHI RAAJIUN
 
P
 
ATC, TAZARA...wafanyakazi wana hela sana; ajabu watakwambia hawajalipwa mishahara miaka mitatu
 
Leo siku ya wanawake duniani, tuwapongeze hata mashujaa ambao ni silent heroes na heroines wanawake waliotangulia mbele ya haki.
Hongera sana shujaa huyu Mwanamke.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…