Yeah. Ni mshiriki wa Segerea SDA church. Sadly miaka mwili iliyopita alimpoteza mwanae wa kiume " Jason Mtsimbe" alifia huko ughaibuni ila aliletwa na kuzikwa hapa. Bila Shaka alikuwa ndiye first born wake.
Mkuu Maxence Melo!, this is shocking news to me, taarifa hii sikupaswa kusomea JF, nilipaswa kuipata in box!.
Sanctus alikuwa patner wangu kwenye baadhi ya projects zake.
Huyu ndie aliongoza ile kampeni ya Kumuenzi Regia Mtema. Huyu ndie alimbeba Le Le Mutuz pale ofisinini kwake!, ni mtu wa pili kunipandisha Range Rover Sport baada ya ile ya Range Rover Autobiography ya Wakili Beredy ambayo ni custom made na kuwa delivered by BA Cargo, ile 2005, Range Sport ya Sanctus Mtsimbe ya 2007 ndio ya pili mimi kuipanda.
Kuna baadhi ya vitu mimi na Sanctus Mtsimbe tulifanana na kuna vingine tulitofautiana, tulifanana kupenda vitu vizuri,kamagari,gari zuri,kama suti, suti kali,barber shop kila wiki,kama ni totoz, totoz bomba, ofisini kwake, wasanii maarufu wa kike ndio wanapishana, usiseme!, tofauti yetu mimi yeye mwenzangu aliwaheshimu, ilikuwa ni mahusiano ya kikazi tuu, wakati mimi ilikuwa ni "Kazi na Dawa".
Kufahamiana na Sanctus.
Mimi japo ni Msukuma, na sisi Wasukuma tunasifika sana kwa ushamba, mimi naomba kukiri kuwa japo mimi ni Msukuma wa mjini, niliyezaliwa mjini, nikasomea mjini, Dar na Arusha, ila ushamba wa Kisukuma wa kuchanganyikiwa na "vitu white" pia bado ni mshamba wa ma ndinga na big bikes!.
Mwaka 2005 kampuni ya magari ya Land Rover walitoa 1st edition ya Range Rover Sport, washikaji wangu wawili, Bered na Johnson, wakazama London, waka press order Range Sport 2, custom made Autobiography zikatua nchini kwa dege kubwa la cargo la BA, Boeng 747 Jumbo Jet, ukazishusha hizo ndinga mbili!.
Baada ya hao madogo wawili kushusha hizo ndinga, Range Sport ikaingia kwenye limelight, mtu ukiona ngozi nyeusi inavuta Range Sport, unapata dukuduku na mshawasha wa kumjua huyu jamaa ni nani?
2007, kuna event fulani pale British Council, Sanctus alikuwa anafanya presentations fulani kuhusu Simba Net, mimi nikachangia kitu, wakati wa tunatoka Sanctus aniuliza Kiti Moto kimefia wapi?!, tuonane tukifufue. Tukaagana, nilipomuangalia, akavuka barabara amepaki Range Sport pale CRDB, Holland House!. Nilisimama nikimkodolea macho mpaka anaishia!.
Toka hapo tukaanza urafiki, akanikaribisha Simba Net, tukaa chini kuanzisha studio, akaanzisha Jason Production, alinikaribisha studio yake niliitumia bure pale Tancot House wakati mimi nikiwa Mtaa wa Mkwepu,
Wakati wa kipindi kile cha kukaza kwa vyuma, mimi vilinikazia sana hadi vikaumana, hivyo kulazimika kufunga ofisi ya Mkwepu, huyu jamaa alinibeba kwa muda pale ofisini kwake, ndipo nikagundua kumbe yale makeke yote na ma babez ya Le Mutuz, jeuri ile huyu jamaa ndio mfadhili na mhifadhi Mkuu wa LE MUTUZ SUPER BRAND.
Jana tarehe 11 oct, Waziri wa Habari,vijana,Utamaduni na michezo Dr. Fenella Mukangara,alizindua ile filamu inaliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, Yaani Wekeza inalipa, iliyoigizwa na wasanii wakali kutoka East Africa, yaani Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi na Tanzania. Hii habari imechapishwa na...
Sanctus Mtsimbe alikuwa always very smart and formal, sikumbuki kumuona event yoyote bila suti, nimi nilikuwa sometimes smart, sometimes casual and sometimes niko rough!.
One day nimevuta mpunga wa maana kwa Boss Mtsimbe, nikaamua huyu binti ni ama zake ama zangu!, binti akakubali zoezi la kazi na dawa, baada ya kazi, twende mahali tukapate dawa, siku hiyo Ijumaa, tumemaliza mapema, nikamwambia binti mimi natangulia chini, basi nikashuka chini na kusubiria kujibebea kama nimeokota!.
Binti akashuka na funguo za ndinga yake mkononi akasema kwa vile yeye ni star, kila mtu aende na usafiri wake tukutane sehemu, ili usiwape watu faida bure ya kupata kitu cha kusema!. Mrembo kwenda kwenye gari kumbe ni yeye ndiye ana vuta ile Range Sport ya Boss!. Hapo kuna cha kuuliza tena!, ni heshima adabu!. Kumbe ulikuwa wasiwasi wangu tuu, Boss Mtsimbe ni mtu smart, muadilifu na mchaMungu!, ni msafi kwenye muonekano, msafi kwenye mawazo, msafi kwenye maneno, msafi hadi kwenye matendo!, hanywi pombe, havuti sugar, sio mtu wa kujirusha, he was really smart kila Idara, yeye ni kazi kazi, sio akina sisi wa kazi na dawa!.
Baada ya project ya DSE kukamilika akafungua TV yake.
Kwa JF Sanctus Mtsimbe alikuwa ni Mwalimu.
1. Kwanza alisisitiza connectivity, watu wawe connected, ni kupitia connections na connectivity aliamini kila mtu unaweza kufanya kila kitu kwa kujiunga na wengine kuunganisha uwezo na kutenda. Hivyo pale ofisini kwake alisaidia wengi kushinda tenders. TPN, Jamiiforums na Michuzi Blog Yakabidhi Tena Misaada Ya Wahanga Wa Mafuriko
-https://www.jamiiforums.com/threads/uthibitisho-kuwa-una-una-uwezo-wa-kufanikiwa-katika-chochote.681388/
- Jinsi ya Kupata Mtaji kwa Bila Dhamana Kupitia DSE
2. Alisisitiza Afya Bora, ili ufanikiwe ni lazima uwe na uwezo wa kufanya kazi hivyo alisisitiza sana afya bora, alikuwa hali ovyo ovyo, hanywi pombe, havuti sigara, na ile starehe nyingine... yeye wala, ni kazi tuu!
You may think that you do not have the chance to be a millionaire and wish that someone in your next generations will be successful. You make sure that next generation have the adequate education to be successful. On the process of your child growing up, you often tell him/her that they must...
5. Alipenda vitu vizuri, wakiwemo warembo. Kuna wanaume na mababa wengi wanapenda warembo, kumbe ukweli hao watu sio wanawapenda warembo, ni wanawahitaji wawatumie hivyo wanazuga kuwapenda!, lakini Sanctus Mtsimbe aliwapenda kwa dhati ili kuwasaidia na sio ili kuwatumia!. Shuhudia
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.