Tribute to Silent Heroes!. Hongera “Idara” Kuhudumia Wastaafu Wake Till Death!”. Jee Huu Sio Ubaguzi?. Why Only Some are Cared to Death but not All?!


Mkuu Mayalla, kwa vile kuandika ni maisha yako na maisha yako ni kuandika, huna budi kuandika kwa kuzingatia punctuation rules. You do have some room for improvement in this regard. (No offense intended! Mimi ni muumini tu wa Elimu ni Bahari.)

I believe the following Punctuation Guide is comprehensive enough to help you gain a sufficient mastery of the punctuation rules.

 
..Pole sana kwa msiba wa mama yako mpendwa (Bibi yangu).

..Wastaafu hawawezi kuwa
sawa mkuu....kama huo usawa upo basi ni nadharia tu, ila kiuhalisia hakuna kitu kama hicho.
 
Nitashangaa sana kama Kaka Paskali hujawahi kukisoma kitabu cha "The Animal Farm" by George Orwell.
 
Paskali, pole sana kwa msiba mzito wa mama yako mzazi.

May her soul rest easy in peace.

[emoji120]
 
Kuna ukweli mtupu kwenye hii thread. Hasahasa askari wastaafu wa JWTZ, ambao hawana hata bima ya afya. Wanahangaika sana kwenye matibabu. Hata waliopo tu sasa kazini, matibabu kwao ni janga kuu.
 
Kuna ukweli mtupu kwenye hii thread. Hasahasa askari wastaafu wa JWTZ, ambao hawana hata bima ya afya. Wanahangaika sana kwenye matibabu. Hata waliopo tu sasa kazini, matibabu kwao ni janga kuu.
Kama ni kweli Basi huo ni upumbavu...jwtz anakosaje bima!!!?
 
kwanza nikupe pole kwa msiba.....

kama ambavyo unakiri hukujua alikua nani basi huna haki ya kuhoji kwann kalipwa/alikua analipwa kiasi kikubwa inawezekana mwisho wa jua yako ilikua ni nishani mengine waachie wahusika.
 
Poleni Sana watoto wa marehemu Mama Kundi.Tunamwombie apate pumziko la Amani.(RIP mama Kundi).
Hiyo rambirambi nono,labda ililetwa kuwapo pole ndugu zako ambao bado wapo kwenye kitengo,(kwa maana wewe Pascal umetuthibitishia kuwa hukujiunga na fani za wazazi wako).
Ninaunga mkono hoja, Mamlaka husika,ipitie upya sheria ya kuwalipa (viongozi wakuu wa Serikali) pension asilimia 80 ya mishahara ya viongozi waliopo madarakani,ili iwe kwa watumishi wote umma.Hata kama watalipwa asilimia 50 ya mishahara ya sasa( kwa watumishi wa ngazi husika).
Wastaafu tuna hali ngumu
 
Pole sana mkuu, ulichoeleza ni ukweli dhahiri.
Pole Pascal kwa msiba. Haya mambo ya kulipana mafao kidogo au kikubwa yanatuhusu sote kama nchi na wala si la mtu mmoja au kikundi cha watu. Kimsingi si rahisi watumishi wote wakapata treatment sawa, kama ilivyo watushi wa serikali kazi na majukumu yao yanatofautiana. Ushauri wangu serikali iandae utaratibu ambao utafanya pensheni za watumishi zisiwe dormant bali ziwe zinaongezeka kwa kiasi fulani kulingana na hali ya maisha au muda.
 
Dah! Kweli Mwandishi ni Mwandishi tu! Umesimulia kama stori, kumbe ndani yake mhusika ni mama yetu.
Pole sana Bro kwa kufiwa na Mama. Na ni jambo la kushukuru umezifaidi busara zake mpaka wakati huu.

Binafsi namshukuru Mungu, Bimkubwa wangu aliyezaliwa mwaka 1935 bado anaendelea tu kudunda huku milimani, ingawa na maradhi nayo ya uzeeni hayamuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…