Tribute to Silent Heroes!. Hongera “Idara” Kuhudumia Wastaafu Wake Till Death!”. Jee Huu Sio Ubaguzi?. Why Only Some are Cared to Death but not All?!

Pole sana Mayala, wafanyakazi wa serikali sidhani kama wanaweza kuwa na upendo kwa serikali ya tz kwa namna wanavyokuwa treated wakiwa kazini hadi wanapostaafu;
Malipo kidogo halafu yanaweza kuchelewa hadi miaka 4 bila mstaafu kulipwa.
Mbunge anakaa bungeni miaka 5 tu analipwa fedha ambazo mstaafu aliyetumikia serikali miaka 35 hawezi hata kwa robo ya mafao hayo!! Shame!
 
Aisee hongera sana kwa umri huo hiyo ni neema kubwa sana. Nina uhakika ukifuatilia mahusiano ya huyo bimkubwa kwa wazazi wake ni Yale yaliyotukuka. Hapa ninamaanisha kuwa wengi wanaoishi miaka mingi ni wale WALIOWAHESHIMU WAZAZI WAO IPASAVYO NA KUWATUNZA. Ukiheshimu wazazi wako kwa dhati tunaamini Mungu atakupa Umri Mrefu hapa duniani.

Wengi wetu sikuhizi tumekuwa tuki argue sana na wazazi wetu, tumekuwa na vifua vya kuwakosoa, hasa tunapokuwa tumetoka mikononi mwao tunajitegemea. Tumekuwa wakali kwa wazazi wetu hadi wanajiona inferior hawawezi kutoa Maelekezo kwakujiamini BALI WAMEKUWA WAKIOMBA( Too Bad).

Hongera Sana kwa Neema hiyo. Jitahidi kumpa Amani afurahi .
 
Pole Sana Pascal . Pia Ushauri uliotoa umeonyesha kiwango kikubwa cha Uzalendo kwa kuwasemea waliowengi. Lakini pia umesema pamoja ya kuwa Baba na Mama kuwa watumishi lakini wewe sio mmoja wao, Mimi ninachoamini ni kwamba AS FAR ULISHAKUWA JWTZ THOSE DAYS BASI WEWE NI MMOJA WAO TU.
 
Mkuu Paskali pole sana kwa msiba mzito wa mama yako mzazi,

May her soul rest easy in peace.
 
Kuna ukweli mtupu kwenye hii thread. Hasahasa askari wastaafu wa JWTZ, ambao hawana hata bima ya afya. Wanahangaika sana kwenye matibabu. Hata waliopo tu sasa kazini, matibabu kwao ni janga kuu.
Wanajeshi wasisibiri hadi wafikishe miaka 55 ndio wastaafu
 
Pole sana Paskali aka Pascal Mayalla kwa kuondokewa.
 
Kuna mtu alileta uzi humu akiulizia umepotelea wapi kumbe ulikuwa chimbo Paskali😆🤣 sawa naona amepata majibu
 
Kuna wananchi na wenyenchi, Hayati Mwl. Julius K. Nyerere alisema hadi segereti alizokuwa anavuta zilinunuliwa na serekali🤣😆
 
Paskali uliwahi kufanya kazi na namba moja mmoja asiyelipa kodi pamoja na kupokea kipato kinene, hivi kweli hukuyaona haya wakati huo hata ukampenyezea chini ya mlango wake kama uliogopa kuminywa? Ungefanya hivyo wakati huo huenda leo ungetangazwa shujaa maana wanaoumia zaidi ni wanaolipa kodi kubwa na mafao membamba tena wanalipwa kwa manyanyaso as if yanatoka mifukoni mwa familia fulani kumbe ni michango yao masikini
 
Idara inastahili pongezi, kwani baada ya Idara kupokea taarifa ya kifo hicho, maofisa wa Idara, walifika nyumbani na kutoa rambirambi kubwa nene ya kutosha kugharimia mazishi.


Polepole Paskali usiseme sana, wanaweza kuirudia hiyo rambirambi ukaikosa

RIP Mama Graciana
 
na sifa za mbunge anaye lipwa hizo, ajue kuandika na kusoma, zaidi awe na ujuzi wa kugongq meza kwa ufasaha wakt wa kuunga mkono hoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…