Trilioni 1.2 za Kujenga Muhimbili Mpya zingeweza kununua machine za MRI & CT SCAN kwa Hospitali zote za Wilaya na Mikoa

Trilioni 1.2 za Kujenga Muhimbili Mpya zingeweza kununua machine za MRI & CT SCAN kwa Hospitali zote za Wilaya na Mikoa

Nodus

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2011
Posts
398
Reaction score
1,105
Kabla ya kufanya jambo lazima tujiulize kuna ulazima wa kufanya jambo hilo au ni WHITE ELEPHANT project ya kujijengea jina.

Leo hii unataka kuvunja na kujenga Muhimbili upya. Sikatai kuwa baadhi ya majengo yanahitaji ukarabati lakini je kuna haja ya kujenga ipya hospitali?

Dar es salaam haina uhaba wa Hospitali. Pia serikali imewekeza vizuri sana kwenye Hospitali za Wilaya na Mikoa, karibu kila wilaya na Mji una hospitali mpya.

Kwa sasa investment inabidi iwe kwenye utoaji huduma haswa za kibingwa.

Kwa nini msiweke Neonatal ICU (ICU za watoto wachanga hasa hasa Watoto Njiti) zilizokuwa fully equiped sio ICU uchwara nchi nzima?

MRI ni Bilioni 1.5 - 3 TZS na CT Scanner 0.9 - 1.5B, kwa maana hiyo Hospitali zote za wilaya 195 na mikoa 30 nchi nzima zinaweza kuwa na Machine hizi na tukawa miongoni mwa nchi chache Afrika kufanya hivyo.

Muhimbili mpya ni WHITE ELEPHANT project ambayo haitatui maswala ya muhimu katika sekta ya afya haswa kwa Mkoa wa Dar es salaam.

Huwezi kutatua changamoto za Afya kwa nchi kwa kujenga hospitali moja.

Hospitali za kanda na kitaifa pia na mikoa zina shida hiyo hiyo, madeni kibao ya wazabuni, wafanyakazi, TANESCO ambao hawajalipwa lakini wanakimbilia kujenga wodi na majengo mapya.

Kwa nini msiboreshe huduma kwanza. Jengo si kitu kwenye hospitali, weka vifaa vya kisasa, huduma zitolewe kwa viwango. Majengo ni kuwafurahisha ambao hawajasoma tu.

Soma pia
 
Back
Top Bottom