Trilioni zetu 360 zipo wapi? Leo Bunge zima linapiga makofi kwa Trilioni 1.3!

Trilioni zetu 360 zipo wapi? Leo Bunge zima linapiga makofi kwa Trilioni 1.3!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Luhaga Mpina: Trilioni Zetu 360 Zipo Wapi? Bunge zima linapiga makofi kwa Trilioni 1.3.

"Tunazo trilioni 360 zimeshikiliwa na Mahakama uamuzi haujatoka, nilitegemea kwenye mpango hapa isemwe hela hizo ziko wapi. Leo bunge zima linapiga makofi kwa Trilioni 1.3 tulizopewa na IMF mpaka mikono inauma!

"Bunge halijaumia, Serikali haijaumia, kama tatizo ni Bodi za Rufaa za Kodi kukosa wataalamu, si waajiriwe wataalamu kutoka nje?

"Tuna kampuni 504 yenye miamala zaidi ya Trilioni 105 kwa mwaka, uwezo wa TRA kukagua makampuni haya ni 1% kwa mwaka, hawana wataamu wala fedha na hawezi kukagua, hivyo hatuwezi kupata kodi kwenye makampuni haya, fedha za Watanzania zinapotea.

"Haya yote hatuoni kama ni shida wala hatupati hasira katika hili, lakini tukiletewa hata bilioni 5 hapa tunafurahi kwelikweli. Nilitegema hata mikataba mibovu na ya kinyonyaji nchini kama ya TRA na SICPA ingezungumzwa Bungeni kuwa inaenda kufutwa mara moja na hivyo kusadia kupata mapato mengi ya serikali.

"TR anasimamaia Mashirika ya Umma 237 ambayo yanategemea ruzuku kutoka Serikalini, hayana mtaji na hayatekelezi majukumu yake sawa sawa. Kwanini mpango hauzungumzii juu ya kuyapatia mtaji mashirika haya ili yafanye biashara serikali iweze kupata gawio kubwa, hela zinazopelekwa kwa ajili ya ruzuku zifanye mambo mengine?

"Msajili wa Hazina anaweza kusimamia makapuni haya kwa 13% tu, hana fedha wala watalaamu, lakini sisi tunaona kukaa na kupanga ni sawa lakini hatufanyii kazi suluhisho la matatizo haya.

"Bado tuna maeneo mengi yenye utoroshaji mkubwa wa fedha, ukienda mipakani madini bado yanatoroshwa, mifugo, mazoa ya uvuvi, misitu na hata wanayama pori bado wanatoroshwa. Mpango unatueleza nini, unaenda kudhibiti vipi maeneo haya ili tuzidi kupata mapato?"
 
content imeshiba... hizi ndio akili zinazopaswa kuwepo bungeni na kufanya mijadala na sio waongeza idadi wanaosubiri muda ufike wakunje posho na kuingia mitaani.

Taifa linahitaji critical thinkers na ujasiri na sio tena mizaha mizaha ya siasa za CCM.
 
content imeshiba... hizi ndio akili zinazopaswa kuwepo bungeni na kufanya mijadala na sio waongeza idadi wanaosubiri muda ufike wakunje posho na kuingia mitaani.

Taifa linahitaji critical thinkers na ujasiri na sio tena mizaha mizaha ya siasa za CCM.
.
20230502_160005.jpg
 
Huyu wa kwenda kupima samaki?
Nadhani kuna maslahi fulani wamemnyima ndio maana ameamua kama mbwai iwe mbwai
Huna akili, au wee ni kajamaa pengine kanachuo au uko mtaani tu na ujinga wako.


Sheria inasemaje kuhusu upimaji wa Samaki??.



Ilo bichwa kafugie minyoo
 
Huna akili, au wee ni kajamaa pengine kanachuo au uko mtaani tu na ujinga wako.


Sheria inasemaje kuhusu upimaji wa Samaki??.



Ilo bichwa kafugie minyoo
Sijamaanisha juhudi zake hazionekani au haishauri vizuri serikali ila juhudi hizi pia inaonyesha kwasababu wanasema ni sukuma gang
Kuwa na akili na kutokuwa na akili ni wewe na akili yako au nyuzi zako za kula kimasihara na unavyojisifia handsome inakupendezesha wewe na sisi tunakuona punga, usimuundermine mtu, hoja inajibiwa na hoja
 
Back
Top Bottom