Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,292
- 10,842
Kipigo cha mbwa koko.NEC kuweni makini, Chadema wamesha ona kipigo kizito ndani ya sanduku la kura...
Kura zihesabiwe hadharani kama za maoni za CCMNEC kuweni makini, Chadema wamesha ona kipigo kizito ndani ya sanduku la kura wanatafuta mtu wa kumrushia Lawama msipoangalia wanaweza susia uchaguzi dakika yoyote kutoka sasa ili Lawama ziwe juu yenu.
Waache unafiki,sisi ni watanzania hatujaridhika na kinachoendelea hapa kwetu wao akina nani hadi watusemee?Asasi ya Ushirikiano wa Siasa,Ulinzi na Usalama (TROIKA) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeridhishwa na mazingira ya hali ya siasa nchini Tanzania yanaruhusu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Octoba 28,2020 na kwamba wataendelea kufuatilia mazingira ya uchaguzi huo.
Akizungumza katika Mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema TROIKA imekuwa ikifuatilia kwa ukaribu tangu awali mchakato wa uchaguzi hapa nchini na kwamba imeridhishwa na mazingira ya amani yaliyopo hali inayoruhusu uchaguzi huo kufanyika.
"Leo katika mkutano wangu na TROKA ulifanyika kwa njia ya mtandao mwenyekiti wa TROIKA ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Botswana Dkt. Lemogang Kwape ameoneshwa mazingira ya hali ya siasa nchini Tanzania yanaruhusu kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Octoba 28, 2020 na kwamba wataendelea kufuatilia mazingira ya uchaguzi huo," Amesema Prof. Kabudi
Prof. Kabudi ameongeza kuwa ni kwa mara ya kwanza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ipate uhuru kwamba uchaguzi huu unagharamiwa kwa fedha ya walipa kodi maamuzi ambayo yamefanyika kwa kutambua kuwa demokrasia ndio jambo kubwa katika uhai,utashi na kielelezo cha Taifa ambalo ni huru kama ilivyo Tanzania.
Kuhusu waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi mkuu wa Octoba 28, Prof Kabudi amesema TROIKA imefanya tathimini ya awali ya hali ya usalama na kisiasa na kwamba Tanzania inategemea kuwapokea waangalizi kutoka Umoja wa Afrika na wale wa kutoka katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala za hati za utambulisho za Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Sarah Gordon-Gibson.
Katika mazungumzo yao Prof. Kabudi amesema WFP imekuwa ni miongoni mwa mashirika ya Kimataifa ambayo yanaushirikiano mzuri na Tanzania ambapo kwa mwaka 2018 WFP imenunua tani 160,000 za nafaka na 2019 wamenunua tani 36,000 zenye thamani ya shilingi bilioni 21 fedha ambazo zimesaidia wakulima wadogowadogo katika kuboresha kilimo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Sarah Gordon-Gibson amesema wamejadiliana namna ya kuendeleza ushirikiano baina ya pande hizo mbili hususani kusaidia wakulima wadogowadogo nchini kuboresha kilimo,kuboresha mazingira ya lishe na kwamba shirika hilo lina mpango wa kuongeza msaada wanaoutoa kwa Tanzania.
View attachment 1607424
Na wewe tengeneza troika ya kwako uwaweke akina mbowe na lissu.TROIKA imejaa akina Museveni, Kagame, South Sudan n.k hapo nchi ya maana ni Kenya pekee(Kenyatta) wengine wote ni hovyo ndiyo maana Kenyata hazungumzii uchaguzi wetu hata kidogo
Sisi Wa Tanzania tumeridhika.....povu ruksaWaache unafiki,sisi ni watanzania hatujaridhika na kinachoendelea hapa kwetu wao akina nani hadi watusemee?
Axis of Evil ..... !!!TROIKA imejaa akina Museveni, Kagame, South Sudan n.k hapo nchi ya maana ni Kenya pekee(Kenyatta) wengine wote ni hovyo ndiyo maana Kenyata hazungumzii uchaguzi wetu hata kidogo
Wajiandae kisaikolojia😁😁😁😁Kipigo cha mbwa koko.
Wacha tukawamalize kwenye sanduku la kuraHongera na pongezi nyingi ziende kwao
Kama ilivyo ada kwenu, Beberu kwenu ndio wa kuamini kuliko hata mbowe mwenyeweNgedere anatoa hukumu kwa Tumbili!
Hakuna chama Afrika kinachoamini na kukumbatia mabeberu kama CCMKama ilivyo ada kwenu, Beberu kwenu ndio wa kuamini kuliko hata mbowe mwenyewe
Na wewe ni mjinga?Hakuna chama Afrika kinachoamini na kukumbatia mabeberu kama CCMView attachment 1607489