DHANA YA UBEBAJI MIZIGO KWA MUJIBU WA SHERIA ZA TANZANIA Je, sheria inasemaje kuhusu kubeba mizigo? Je, ni kosa kutumia gari langu kubeba mizigo? Kuna sheria mbili tutakazoziangalia hapa, nazo ni Sheria ya Usalama Barabarani sura ya 168 ya sheria za Tanzania, na kanuni za SUMATRA za usafirishaji mizigo za mwaka 2012 KANUNI ZA SUMATRA [TRANSPORT LICENSING (GOODS CARRYING VEHICLE) REGULATIONS 2012 Kifungu cha 2 cha kanuni kinatafsiri gari gari la kubebea mizigo (Goods carrying vehicle) kama gari ambalo limetengenezwa au kufanyiwa mabadiliko kwaajili ya kubebea bidhaa au lililotengenezwa au kurekebishwa kwaajili hiyo. Kanuni hazisemi nini maana ya mzigo...