Trucks and truckers special thread. Uzi maalum kwa wadau wa magari ya mizigo na wasafirishaji

haaa,,,we jamaa unamaswali tata!!. mezoeleka fuso yenye diff mbili kuitwa tandam kama alivyokuelewesha jamaa hapo juu.
kipisi ni zile scania ambazo hazina tela.

Pia kuna kipisi cha volvo,daff,actross n.k

Scania ambazo hazina tela zinabebaje mzigo?

Mzigo unakaa wapi kama hakuna tela?
 
Scania ambazo hazina tela zinabebaje mzigo?

Mzigo unakaa wapi kama hakuna tela?
Ndo hizo zimezoeleka kwa jina la kipisi,zenyewe hazivuti tela.
zenye tela kuna pulling,semitrailer n.k
 
LEO NMEJIFUNZA KITU HAPA, NLIKUWA NAJUA TANDAM NI FUSO TU KUMBE HATA SCANIA INAWEZA KUWA TANDAM ILI MRADI IWE NA DOUBLE DIFF

ASANTE SANA JAMIIFORUMS
 
Mkubwa umechoraaaa dah
 
Kuna Siku Niko Iringa Tulikaa Site Kwake Hanspope Nikamuuliza Swali Apart From *DISCIPLINE* Ya Biashara Ya Transport Ni Kitu Gani Zaidi Ya Hapo?

Aliniambia *UKOROFI* 😂
Hakuna Kucheka Na Dereva.

Nachukua siti nitarudi hapa

Huu uzi sikuwahi kuuona
 
Anhaa, Tandamu inaweza kubeba tani 16

Na kipisi umesemq ni gari inayobeba tani 16 kuendelea

Kwa hiyo tandamu ni kipisi?
tandeem (tanadam)ni gari yenye axle mbili nyuma iwe double diff ama diff moja na dead axle pia yaweza kuwa inavuta trela(pulling) ama isiyovuta trela.

neno kipisi linatumika kwa kumaanisha gari ibebayo 10tons na kuendelea ila isiyo na trela.

mfano mtu anaweza kusema nimechukua kipisi cha 10tons ama nimechukua kipisi cha tandeem(tandam)

sasa akisema kipisi cha 10tons huwa ina maana ni single diff( yenye diff moja nyuma)
 
tandeem (tanadam)ni gari yenye axle mbili nyuma

neno kipisi linatumika kwa kumaanisha gari ibebayo 10tons na kuendelea ila isiyo na trela.

Kwa definitions zako, gari hii hapa chini

ni KIPISI ( haina trela na inabeba zaidi ya tani kumi)

na hapo hapo ni tandem (ina axle mbili nyuma).



Kwa hiyo bado unajichanganya. Tandem na Kipisi ni gari mbili tofauti.
 
Kwa definitions zako, gari hii hapa chini

ni KIPISI ( haina trela na inabeba zaidi ya tani kumi)...
hto fuso haiwezi kuitwa kipisi sababu haiwezi funga teller nyingine nyuma hapo ikavuta pulling,,, kipisi ni zile Hozi kubwa kama scania howo nk lakin zinakuwa na body ya moja kwa moja sio ya kupachika

Sent from my Nokia 2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…