Mkuu
Upo sahihi kabisa ,ila watu wameaminishwa tofauti na wanasiasa .
Reli haiwezi kuwa suluhisho la usafiri nafuu kama tunavyoaminishwa , kimantiki reli unaweza kuwa usafiri wa gharama sana kwa baadhi ya vitu , chukulia mfano wa mbao ya makambako, na masoko yake buguruni, ni rahisi.kwa mfanyabiashara kukodi lori ambalo litafika siku ya pili sokoni, kuliko kukodi treni ambayo itachukua hadi wiki kufika sokoni na bado truck itahitajika kupeleka mzigo makambako station pamoja na kuchukua mzigo buguruni Tazara station .
Hata huko USA ,nchi yenye railways network kubwa kuliko zote duniani , bado trucks zina demand kubwa.