True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

117
Babu alinitaka nieleze ukweli ninaoujua juu ya watu wale kupewa pigo lilowalaza hoi vitandani.

Niliinamisha kichwa chini nikiwaza, je nimwambie babu yote yaliyotokea? Je anajua kwamba bibi nae ni mshirika wa walozi? Hapana sitakiwi kusema chochote, niliwaza.

Niseme ukweli babu wale wazee wamenishangaza sana kwa maneno yao kwamba nimefanya watu walale hoi vitandani, kiukweli sijui chochote juu ya mambo hayo, nilimjibu babu.

Ninani ndugu yako kati yangu na huyo mchawi mwenzio anaekudanganya na kukupeleka ukajue siri za watu? Sasa kama unamuona yeye ndo msaada wako sawa, sitokuuliza tena na yatakayokupata atakusaidia yeye, aliongea kwa hasira babu huku akinyanyuka na kuingia ndani kulala akionekana mwenye kuchukizwa ni ubishi wangu.

Nilijiona mpumbav kwa ujinga ule nilofanya, kweli nawezaje kumficha babu mambo ya hatari kama yale?
Nilijilaumu sana.

Kesho nitamsimulia yote, niliwaza huku nikinyanyuka kinyonge na kuingia getoni mwangu huku nikianza kuihisi roho ya kichawi kuanza kuniingia.
 
Endelea acha uvivu kijana

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
118
Ubishi, ubishi.

Ndio ubishi ulianza kuniingia, sasa nilijishangaa yaani mpaka babu namficha kweli? Sasa nimefanywa msukule na yunge, niliwaza huku nikiwa nimejilaza, nilijisemea kukicha tu nampa babu ukweli wote kwani nadhani ameboleka sana.
Siku hii nililala vizuri mno kwani hakukuwa na mauzauza usiku, kulipokucha niliamka mapema na kwenda bombani kuchota maji.

Kama kawaida watu asubuhi ile walikuwepo pale bombani japo si wengi sana, nilipanga foreni kisha nikawasalimia wote kwa mkupuo kwani kulikuwa na jinsia moja tu, ke wote.

Kadri muda ulivyosonga kina mama na wasichana walizidi kuongezeka pale, sasa ilikuwa zamu yangu kuchota, nilikinga dumu 1 usawa wa tundu la bomba kisha nikapanda juu na kuanza kusukuma.

Nilijaza dumu la kwanza, wakati naanza lile la pili nilitahamaki kumwona yunge mkubwa akiwasili na ndoo pale bombani.

Furaha niliyoipata haikuelezeka, nilitoka nduki kumfuata yunge wangu, nilipomfikia nilitanua mikono kwa lengo la kumkumbatia, pasipo hiana naye alifanya hivyo na kunipokea..!
 
Shhhhh!!!Wanasema kama unaona hadithi kasome nyuzi zingine!Ila hapa katupiga na kitu kizito katoka mbio kumkumbatia yunge!!Dah jamaa anatuonaje sijui, nilikua nafuatilia toka mwanzo ila kwa hapo ngoja niwaachie uzi wenu.
Tatizo hawasemi ukweli kama ni hadithi za kutunga
 
Shhhhh!!!Wanasema kama unaona hadithi kasome nyuzi zingine!Ila hapa katupiga na kitu kizito katoka mbio kumkumbatia yunge!!Dah jamaa anatuonaje sijui, nilikua nafuatilia toka mwanzo ila kwa hapo ngoja niwaachie uzi wenu.

[emoji23][emoji23][emoji23] maisha ya kijijini na kukumbatian hadharani
 
Big wa goba
 
Kimsingi binadamu hatutakiwi kufanya kitu bila faida
Naomba kujua unapata faida gani kwa kazi hiyo?

Pili, unapungukiwa nini endapp wenzako wakifatili?
Madam usibishane na watoto jisomee kimya kimya, nakuacha na hii.

"Do not argue with a fool. He will drag you down to his level and beat you with experience."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…