True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

Samahani kwa usumbufu ulojitokeza, nilishindwa kuendeleza stori kutokana na changamoto za kibinadamu, japo nilikuwa natamani nipate muda wa kumaliza stori yangu, ila changamoto zilikuwa nyingi hivyo sikuwa na namna, naweza kuendelea na stori hii mpaka mwisho endapo mtaendeleza sapot zenu katika kisa changu hiki, asanteni sana.
Mzee utaendelea lini? Imekuwa kitambo sana
 
Tunaendelea
Bibi aliingia jikoni akiniacha nimekaa kwenye kivuli cha mwembe, nyumba moja kubwa mgongo wa tembo yenye chumba na sebule, nyumba mbili ndogondogo kulia na kushoto mwa ile nyumba kubwa iliyokuwa imejengwa ikiangalia magharibi, huku zile nyumba mbili ndogo zikitizamana, yakwanza slopu ya bati kama 8 hivi, imepigwa lipu kwa nje hii ilitizama kusini, na nyingine ya ukubwa kama huo ila ya nyasi ikitizama kaskazini, humu ndio bibi aliingia na mda kidogo nikaona moshi unafuka juu nyumba kuashiria moto umewashwa kwa ajili ya msosi,
Basi nikiwa nashangaa mazingira pale bibi alitoka jikoni akanambia njoo hapa mme wangu, basi nikasogea, huku akielekea nyuma ya ile nyumba ya nyasi, tulipofika nyuma ya nyumba, kulikuwa na mahindi yamelimwa kuizunguka mji wote ule,
Ndipo bibi akasema nisaidie kumkamata yule jogoo mwekundu, dah! Mate yalinidondoka palepale ilihali bibi aliona kitendo kile, akasema, usijali mme wangu, yaani hapa nataka mpaka usahau kurudi kwa mama mkwe, kuwa na amani..!
Wachawi mpo?
 
Back
Top Bottom