125
Nawezaje kumficha babu mambo ya hatari kiasi kile? Nilitokwa machozi huku babu akijipa kazi ya kunituliza.
Babu hata usingesema yote hayo, nikata shauri ya kukueleza kila kitu tangu usiku nilipoingia kulala, nipo tayari kukwambia kila kitu pasipo kuficha hata 1.
Nilianza kumsimulia babu kila tukio tangu nilipokutana na yunge mdogo na mkubwa mpaka kuanzisha nao uhusiano na mpaka yunge kunipeleka kwenda kujionea kilinge cha wachawi mpaka niliponusurika kufyekwa shingo na mzee yule wa kiwanjani pamoja na yule mama mnene ambao walikuwa hoi vitandani kutokana na pigo moja hatari la upembe wa yunge.
Katika kumsimulia mkasa ule, nilijipa angalizo kutomtaja bibi hata mara moja, na hatimae nilimaliza kumsimulia babu stori ile na yeye kuanza kunitwanga maswali.
Ebu nambie bila kuficha, ni nani mwingine unaemjua ulimwona kilingeni?
Mimi: mwingine niliemwona pale ni kijana mmoja ambae alikuwepo uwanjani siku niliyoenda kufanya mazoezi pale uwanani.
Niambie ukweli mwanangu, je bibi yako hukumwona kule?
Daah!!!