True story: Babu yangu kama mshikaji wangu

127
Inuka uongeze mkaa kidogo, aliniamuru babu nami nikafanya kadri alivyoniamuru.

Kwahio hata bibi yako nae yupo chini ya amri ya huyu msichana? Sikujua kama huyu msichana ni hatari kiasi hicho na ukimwona huwezi ukamdhania kujihusisha na mambo hayo, nadhani ndio sababu bibi yako anampenda sana huyu mtoto kumbe wanashirikiana, aliongea mfululizo babu huku akionekana kuzama katika fikra nzito.

Ila naona anakupenda sana, kukuonesha siri zake tena za hatari namna ile pamoja na kuwatendea vile washirika wake ili wewe unusurike ni wazi anakupenda mno, alisema babu.

Nilimwuliza babu kuhusu ndoto yangu ya kupaa ambayo nilianza kuiota tangu utotoni, tena mara nyingi hunijia kwenye zile ndoto za kuogopesha sana.

Kabla hajajibu swali langu waliingia wale jamaa walokuwa wanalima, walikuja kujikinga mvua ambayo sasa ilikuwa inachapa vibaya mno.

Vipi rafiki yangu hongo (mapengo) kesho mtamaliza kulima yote? Babu Alimwuliza mmoja kati ya wale jamaa 6 waliokuwa wanalima.

Kesho zidhani babu, majaruba ni makubwa mno!
 

Tunasubiri boss
 
128
Tuliwapa ule mkungu wa ndizi wale jamaa huku babu akiwa amenyofoa ndizi kadhaa kwaajili ya kumpelekea bibi, walizishambulia ndizi zile mpaka wakamaliza zote.

Muda kidogo ulipita na mvua ikakatika, wale jamaa wakaendelea kulima huku babu akinitaka nibebe samaki waliobaki huku yeye akibeba ndizi, alifunga na kufuli kwenye kile kijumba kisha tukainza safari kurudi nyumbani.

Chakula mtakuja nyumbani, huku hii mvua imesha haribu, alisemj babu akiwaambia wale vibarua.

Njiani babu alikuwa akijisifu kwamba hakuna mtu wa kumchezea, nahata mimi mimi mjukuu wake hakuna wakunigusa.

Nawaza jambo moja tu, usije ukaruhusu yule msichana mchawi akupeleke kukutambulisha kwa wenzie kwani itakulazimu utoe kiingilio {kafara} umtoe mtu umpendae ili wamle nyama, alisema babu.

Ilikuwa siku gani msichana alipokupeleka kule? Aliniuliza babu.
Ilikua alhamisi, nilimjibu.

Babu alianza kuimba tena nyimbo za kisukuma kwani tulikuwa tumefika nyumbani.

Wapike vizuri kabisa hao kamongo, eti anajidai halagi wakati hajawahi onja.
 
129
Muda wa msosi ulifika huku wale jamaa vibarua wakiwa tayari washatia timu kasoro mmoja ambae ilisemekana alipata dharura na asingeweza fika.

Tulikula ugali mkubwa, kambale walipikwa vizuri na kamongo ambao sikuwapenda nikingali sijawahi kuwatia mdomoni, ila kutokana na baba na mama kuwazungumzia vibaya pia watu kadhaa nilijikuta namwambia babu mimi sijagi kamongo.

Ebu onja usikie, alinisihi babu nami nikamega kipande kikubwa cha mnofu wa kamongo, nilikipeleka mdomoni huku watu wote wakinitazama waone nitaichukuliaje.

Kweli bwana, alinishinda yule samaki, yaani manofu yake kama unatafuna nini sijui, sikuipenda kabisa, hivyo nilikula kambale kidogo na maziwa kwawingi, wale jamaa walinicheka sana kwa kushindwa kwangu kula manofu yale ya kamongo.

Kabla hatujamaliza kula juma {captain} alikuja pale, hivyo akaungana nasi na kuanza kula.

Baadae waliondoka wale vibarua huku tukibaki mimi, babu na juma ndani ya kislopu changu ambamo tulikaa wakati tunakula.

Vipi kijana kunahabari yoyote umeleta labda?
 
130
Babu alimwuliza juma kama alikuwa na habari yoyote ameleta.

Hapana babu wala sina habari yoyote, nimekuja kupiga stori na kijana mwenzangu hapa kwani anaonekana anapenda sana mpira kama mimi, alijibu juma.

Sawa, mie nawaacha naenda kujipumzisha kidogo, aliaga babu nasi tukamkubalia akaondoka.

Tulipiga stori nyingi na juma hasa za kuhusu boli na mademu pale kijijini huku akinambia kuna demu mkali ambae angekuja pale kijijini siku si nyingi kwani alikuwa anasoma shule moja ya wasichana pale geita mjini, alisema hakuna msichana pale kijijini anaemkaribia kwa uzuri.

Muda ulifika wa sisi kuenda zoezini ambapo j alinitaka tuwahi mapema kwani tukichelewa mimi sitopata namba, tuliondoka tukapita kwao juma ambapo alichukua viatu vyake {kosovo} tukaondoka, ikumbukwe mimi sikuwa na viatu kwaajili ya kuchezea mpira zaidi ya raba nyeusi zenye shingo ndefu zilizoandikwa STAR.

Tulifika uwanjani tukaanza mazoezi ya kupasha miili joto, kisha tukaingia uwanjani, ikafanyika ndiki kwa macaptain wawili, juma na msaidizi.
 
131
Nilishangaa captain msaidizi akianza kuniita mimi upande wake hali iliyopelekea uzuke utani kwa juma kumwambia msaidizi wake kwamba amemuwahi kumwita okwi wake, huku yule msaidizi akisema huyu ni mrisho ngasa.

Baada ya timu kuwa tayari, tulianza kusakata kabumbu huku juma akiwa ameniazimia viatu kwa dogo mmoja aliyekosa namba na kubaki nje kungoja.

Baada ya zoezi tulikusanyika katikati ya uwanja na kupeana mawaidha kama ilivyo kawaida kwa timu za vijijini, nilishangaa kila mtu alikuwa ananitupia macho, wengine walikuwa wanaambizana kwamba huyu dogo akicheza mbele na joji, siku hiyo wale jamaa watakubali mziki.

Juma na wazee kadhaa walitutaka twende tukamwone yule mzee wa jirani na kiwanja kwani alikuwa anaumwa yu hoi kitandani, sikutaka kwenda pale kabisa kwani ni mimi ndio chanzo cha yeye kulala hoi kitandani.

Nilimwita juma pembeni na kumwomba radhi kwamba nisingeweza kwenda pale kwani usiku ulikuwa umeingia hivyo nilitakiwa niwahi nikakoke moto, juma hakuwa na noma aliniruhusu nikaondoka.

Mamaaa!
 
Imeandikwa...waovu hukimbia pasipo kukimbizwa🤣
 
Nawashukuru kwa kuendelea kuifuatilia stori yangu, japo kuna wanasema ni uwongo, sawa sintowajali kamwe kwani wahenga walisema ukibishana na mjinga nawe utaonekana mjinga.

Endelea kuwa nami katika stori yangu hii yenye visa vya kusisimua, kwani naamini mtaipenda tu.
Uchawi,
Mapenzi,
Wivu
Hila na roho ngumu utavipata humu, muhimu ni kuvumiliana tu, nitakapo banana mnivumilie, nikipa tyme kama hivi, nazimwaga, na kwawanaotaka ung'eng'e ntawadanganya, darasa la 7 aafu nikijijini kule kiswahili chenyewe cha wachache mpaka ilifikia muda wananzengo wakawa wananiita kaswahili {mswahili}.

Basi kwa leo naomba tuishie hapa na tukutane 12 asbuhi kabla sijaingia kibaruani.
Alamsik
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…