True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

True story: Jinsi nilivyopambana kutafuta mali za Mjerumani mkoani Morogoro, mauzauza na vimbwanga nilivyokutana navyo

LUWALE

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2016
Posts
236
Reaction score
286
Habarini za leo wanaJF

Niliombwa na baadhi yana JF kutoa ushuhuda wangu kidogo jinsi nilivyopambana kutafuta mali za mjerumani mkoani Morogoro. Hii ni baada ya kuona nikichangia baadhi ya thread kuhusiana na matukio hayo. Ni matukio ya kweli

Ndugu wana JF kwa wale wanaopenda kufuatilia habari hizi basi tutaelezana kwa ufupi tu ingawa nilipanga hapo baadaye kwenye uzee wangu basi niandae kitabu cha kueleza stori nzima ili uwe mchango wangu kwa vijana wanaotafuta maisha.

Stori ilianzia hapa:
Mimi ni Mluguru na kwetu hasa ni Mkuyuni sio mbali sana na Moro mjini. Ila shangazi alikuwa anakaa maeneo ya Mikese pia ni karibu na Morogoro Mjini. stori hii ni ndefu sana ila nitaeleza kwa mukhtasari sana kwa sehemu Nne. Leo nitaandika sehemu ya kwanza, kisha Jummanne nitaendelea na ikifika jumamaosi Ijayo nitakuwa nimetoa Mukhtasari tu.

kama unaenda Morogoro ukifika maeneo ya maseyu upande wa kulia unaanza kuona milima. inaonekana kam haipo mbali na barabara na pia inonekana kama milima ambayo haina miti wala msitu ndani yake. La hasha hali haipo hivyo. ile milima ipo mbali sana na hakuna bara bara ya kufika pale ni macho tu uanona ipo karibu. ukianza kutembea kwa njia za pale mpaka kufika kule sio chini ya dak 40 ndio utafika pale na pia kuna miti mikubwa mingi sana na msitu mkubwa sana. kuna wakati huwa kunatokea moto katika ile misitu na wakati huo kunakuwa sio msitu mkubwa kwani sehemu nyingi zinakuwa zinaonekana.

Mjomba wangu alikuwa anfanya kazi Forest na walikuwa wanakwenda kulinda watu wasichome mkaa. siku moja mjomba akaenda katika moja ya milima ile na walikuwa maofisa 3 wa forest. walipofika pale basi mjomba wangu akawatangulia mbele na kuwaacha kama mita 15 hivi, kisha wenzake wakasita kwenda mjomba wangu akasogea zaidi na kisha mjomba akasikia kelele za wenzake wakimwambia akimbie kwani kuna nyoka mkubwa sana juu ya miti ile. Mjomba wangu alishindwa kutembea maana alijisikia kuishiwa nguvu kabisa maeneo yale na kuanguka chini. Wenzake wakaosogea mbali sna na mahali hapo huku wakiangalia nyokoa mkubwa sana aliyetanda miti 6 akiwa anaondoka pale taratibu, baada ya muda nyoka yule akatoweka bila ya kumdhulu mjomba wangu aliyekuwa ameanguka chini ya ile miti.

Wenzake wakamtoa mahali pale na kumsaidie na kisha akawa sawa na alismuliwa kuhusu lile tukio. mjomba akasema, "Nilivyofika mahali pale ghafla pakawa pana baridi kali sana na kuisi kuishiwa nguvu pamoja na pumzi, nilisikia mkipiga kelelele lakini sikuelewa chochote baada ya hapo sikujua kilichoendelea".

Ila nitaomba mlima huo nisiutaje ila ni mmoja unaonekana hata ukipita barabarani kwenda au kurudi Moro.

Lile tukio la mjoma wangu lilinifanya nijiulize maswali mengi sana, basi nikawa naenda kwa shangazi yangu mara kwa mara katika maeneo yale.

kumbe katika kile kijiji wanafahamu nini kimo katika milima ile, nilanza kusikia bahadi ya vijana wa pale kuhusu watu maalumu kwenda katika mmoja wa milima ile na kupata mali.

Nikaamua kwenda kukaa kwa shangazi yangu muda wa wiki 3 ili nifanye uchunguzi wa kina kuhusu kijiji kile na mali kwenye mmoja wa mlima ule.

Nikapewa story hii kwa siri . " "watu wametajirika wamejenga majumba kwa ajili ya mali zilizomo katika milima ile, mle ndani kuna maji ya mercury"

Nilishtuka sana kusikia hivyo basi na mimi nikaanza harakati za kujitosa

Nitaendelea
 
Inaendelea

Basi bwana nikamuaga shangazi naenda mlimani kufata mali na utajiri, nilivo fika mlimani nilipigwa na butwaa kuyaona maji ya mercury, nikataka kuyanywaa ile nataka kunywa tu nikasikia sauti unasema kwa kipogolo. kazopata, kazojidai, kazojenga, nilistukaaa sana.
 
Inaendelea..
Basi bwana nikamuaga shangazi naenda mlimani kufata mali na utajiri, nilivo fika mlimani nilipigwa na butwaa kuyaona maji ya mercury, nikataka kuyanywaa ile nataka kunywa tu nikasikia sauti unasema kwa kipogolo. kazopata, kazojidai, kazojenga, nilistukaaa sana.
Mkuu acha kutuzingua, unapost fupii sana. Haipendezi, umeamua kutupa stroy basi tupeee. Ya nini kupeana arosto na jua lote ili bana
 
Sehemu ya pili

Nikajrnga ukaribu na majirani wa shangazi yangu na kisha hata kujua baadhi ya watu wanaokwenda kwenye ule mlima na kupata hiyo mercury. Nilithibitishiwa kuwa mercury watu wanaipata na nikapewa majina ya watu ambao wamenufaika na mercury hiyo na kwenda kuishi mjini.
Basi nikajawa na tamaaa na hamasa uwenda nami nikawa mmoja wa wanufaika hao. Nilipeleleza mpaka nikaijua nani mkuu wao.

Nikajipiga kifua siku moja nikamuingia mzee yule. Nikamsemesha kwa kiluguru, namimi niwe miongoni mwa watu watakaokwenda kutafuta mercury iweze kunisaidia, mzee alikataa akaaema hakuna kitu kama hicho wao wanaenda kule kwa shida zao na sio utajiri.

Sikukata tamaa, nikamfuata mwingine ambaye alinielekeze niende kwa yule mzee kwani ndio mkuu wa kikundi hicho cha kimila. Akaniambia fanya subira tu kwa siku moja mbili hautoweza kukubaliwa. Huyu mzee ndio mganga wa hapa kwetu na anatambulika na bibi wa milima ile. Basi siku ya kufuata dawa nitakwambia. Hatusemi mercury ni dawa ndio lugha inayojulikana na bibi wa mlima ule.

Nikaendelea na miangaiko yangu lakini nilikuwa sipungui kijiji kile kuomba ukaribu. Siku akaniambia dawa tutafuata alhamisi ijayo usiku. Ila usimwambie mtu na wala usionekane maeneo ya kijijini muda wa usiku.
Nikamuuliza mnafanyaje? Na hiyo dawa ipo maeneo gani katika mlima? Lengo la hili swali ni kujua formula na kupambana mwenyewe bila woga.

Akasema tunaenda na mzee usiku mkubwa na tunaimba nyimbo pale karibia na pango na kupiga ngoma mpaka bibi atuurize shida zetu. Akasema bibi ndio jini anayelinda mali zile....
 
Back
Top Bottom