Yule binti aliye mchoma kisu gen.mmewe wake wa zamani ambae wamezaa nae watoto wawili walio kuwa wakisomeshwa na gen. Tewete nae yupo jela baada ya kumchoma mwanaume mwingine kisu baada ya kumfumania akila bata na Aisha. Ni mwaka wa tatu sasa mme wa Aisha yupo jela na sasa Aisha nae anamfuata mmewe huko huko jela baada ya kumuua gen. Tewete fundi wa madege ya jeshi.
Watoto watateseka sana baba jela mama nae jela kwa kuchoma visu.
Source: Masao bwile.
Fidel80 ni kweli umepost thread ambayo haiko straight kueleweka kwa urahisi, ndio maana tufike mahali tukubali, kazi ya kutoa habari nayo ni kazi ya watu!
Issue yenyewe ni simple tuu na iko hivi.
Mwanamke mmoja aitwa Aisha ambae ameolewa na kubahatika kupata watoto wawili na mumewe. Miaka mitatu iliyopita, mumewe na Aisha alimfumania mkewe (Aisha), hivyo kumchoma kisu mgoni wake, kitendo kilichompeleka jela mpaka sasa bado yuko jela akitumikia kifungo cha miaka mitatu.
Wakati mume wa Aisha akiwa jela, ndipo Aisha akapata mwanamume mwingine msamaria, aliyekubali kuwa mpenzi wake, na kukubali kuwasomesha wale watoto wawili wa Aisha, ambao baba yao yuko jela!. Mpenzi huyo wa sasa wa Aisha ndio huyu Mjeshi, Gen. Tawete!.
Aisha nae, alimfumania Gen. Tawete na mwanamke mwingine, hivyo akamchoma kisu kilichomuua Gen. Tawete, hali iliyopelekea Aisha kupelekwa gerezani, ambako hatimaye atahukumiwa kifungo na huko kifungoni atakutana na mumewe ambaye ndie baba watoto wake!.
Mtoa mada akasisitiza sasa watakao teseka ni watoto, kwani baba yao alipokwenda jela, msamaria Gen. Tawete, ndiye aliyemtunza mama yao, kuwatunza wao na kuwalipia ada, lakini sasa mama yao, amemuua huyu msamaria hivyo sasa hawana msaada wowote, kwasababu baba yuko jela, mama yuko jela msamaria ndio huyo kauwawa, hivyop kwao ni mateso mara 3!.
My Take.
Hii ni story ya kusikitisha na kuhuzunisha, kwanza kwa Generali wa jeshi kuuliwa kwa kisu kama kujinja kuku na sio tuu kuuliwa kwa kisu tuu bali muuaji mwenyewe ni mwanamke!, hiki ni kifo cha aibu, achilia mbali aibu ya General kufia kwa kimada, wakati yeye ni mtu wa heshima zake na hadhi ya juu kabisa katika jamii!.
Pili huyo Mwanamke Aisha, japo kwanza atafunguliwa shitaka la mauaji, akipata wakili mahiri, shitaka hilo litageuzwa kutoka murder (kukua kwa kukusudia) mpaka manslaughter (kuua bila kukusudia) na wakili huyo akiitumia vizuri defence ya 'provocation' na akawatumia madaktari bingwa wa afya ya akili, kuthibitisha hiyo 'provocation' ilifikia kiwango cha kusababisha 'insanity', na kuprove beyond reasonable doubt kuwa wakati anamchoma kisu, she was insane!, huyo mama ataachiliwa kwa compassion ya kuwenda kuwalea watoto wake wanaomtegemea maana na baba yao yuko jela!