True Story: KISENGE

True Story: KISENGE

mshana jr kula [emoji109] nyelwa kissenge rip mi mzee wangu kabisa mimi ni last born wake,please have respect to him wakuu
pole..... !!! jaman tuweke heshima kwa marehemu tume joke vyakutosha mwacheni mzee huko alipo
 
Tangu unaingia Jf ulikuwa unafanya nini mpaka leo ukafikiria kutuletea habari za kisenge?!
 
unajitahidi Kutoa historia,ila hakuwahi kuwa katibu wa chama singida,alikua RDD now days wanajulikana kama RAS
Ni kweli, hapa Morogoro ukisema unataka kwenda RDD, unapelekwa kwa Makonda wa Morogoro
 
Nyelwa Kisenge alikuwa DC huko Mbulu miaka ya 1980s, alikuwa DC mkali na mchapakazi sana. Alikuwa pia mfuatiliaji sana na aliibadilisha sana Mbulu. Miaka hiyo kulitokea ugonjwa wa Tauni na akaagiza kata 3 ziwe chini ya karantini.

Katika kutekeleza maagizo yake, Katibu Tarafa mmoja aliitisha mkutano wa hadhara na kuanza kuwaambia wananchi..

"Leo nimekuja kufuatilia maagizo ya Kisenge! Si wote mlisikia maagizo ya Kisenge? Nani hataki kutekeleza maagizo ya Kisenge? Lazima mtekeleze maagizo ya Kisenge! Kama mna malalamiko si kwangu, ni ya Kisenge!

RIP Mhe. Nyelwa Kisenge, pia alipata kuwa katibu wa chama Singida, Shinyanga, n.k. na ni mpare wa Usangi.

Poleni familia..
Muulize jepesi akueleze pia Jina simbangufira ili story zako zikamilike!
 
Ndugu zangu,
Mimi nilisoma na Hardy Amos Kissenge St. Joseph's Convent School Dar es Salaam lakini toka tuachane mwaka wa 1970 hatujaonana.

Nikafanyakazi na dada yake Rachel Amos Kissenge Bandarini katikati ya miaka ya 1970 na Rachel pia sijamuona miaka mingi sana.

Wote hawa walikuwa watu wema sana.

Ajabu nilikuwa karibu sana na Rachel kuliko nilivyokuwa na kaka yake na alikuwa mzungumzaji wangu sana na kupitia kwake nilikuja kuwajua vijana wa Kipare walioshika madaraka ya juu katika serikali ya Mwalimu Nyerere.

Wakati natafiti kitabu cha Abdul Sykes nilikutana na Amos Kissenge na hapa chini nakunyambulieni Mzee Kisenge kama anavyotokea kitabuni:

''Baada ya kupata kikundi kidogo cha wanachama, Haruna Taratibu alipiga simu makao makuu ya TANU na kuzungumza na kaimu katibu, Elias Kissenge akaomba ruhusa ya kufanya uchaguzi.

Kissenge hakuweza kutoa uamuzi wowote wa maana kuhusu tatizo la uongozi wa TANU Dodoma.

Taratibu alifanikiwa kumpata Kambona ambae aliidhinisha uchaguzi ufanyike kwa shuruti moja la kuwa Hassan Suleiman na Ali Ponda waruhusiwe kushiriki na kugombea uongozi wa chama.

Kusisitiza kwa Kambona juu ya uongozi wa zamani wa TAA kuongoza chama kipya huenda kulishawishiwa na mafanikio ya zamani ya uongozi wa Hassan Suleiman mbae alimfahamu huko Dodoma wakati Kambona alipokuwa mwalimu akifundisha Kikuyu Secondary School.

Kwa bahati mbaya, wanachama wa TANU waliokuwa wanainukia na chama pale mjini Dodoma waliwaona Hassan Suleiman na Ali Ponda kama wasaliti kutokana na kutokushirikiana na wenzao katika kuanzisha TANU.''
 
Back
Top Bottom