Trump aanza kudhibiti mamlaka ya Elon Musk

Trump aanza kudhibiti mamlaka ya Elon Musk

Tulisema Hapa hao hawana muda watamwagana tu Elon Musk amekuwa front sana utadhani yeye ndio POTUS, The presidency is a jealous institution,
Never outsmart your master
 
Musk ana cheo Gani hapo white house?
Elon Musk ana cheo cha mshauri maalum wa serikali chini ya utawala wa Rais Donald Trump amepewa jukumu la kuongoza Idara ya Ufanisi wa Serikali (DOGE), ambayo inahusika na kupunguza matumizi ya serikali.
 
Rais wa Marekani Donald Trump alifanya mkutano na Baraza lake la Mawaziri na kusema kwamba usemi wa mwisho juu ya sera ya wafanyakazi utatolewa na wakuu wa mashirika ya shirikisho, sio mkuu wa DOGE Elon Musk.
Vyombo vya habari vya Reuters, Politico na CNN vimeripoti ripoti hii, wakinukuu vyanzo vya kuaminika vya serikali.
Mkutano wa Trump na viongozi wa mashirika ya shirikisho ulichukua dakika 90 na haukuwajumuisha waandishi wa habari. Hata hivyo, vyombo vya habari vinaeneza habari vikiwanukuu viongozi walioshiriki mkutano huo..
Rais Trump amesema anaunga mkono kikamilifu juhudi za Elon Musk za kupunguza idadi ya wafanyakazi na matumizi katika serikali ya shirikisho. Lakini Trump alisema kuwa Idara ya ufanisi wa Serikali, inayoongozwa na Musk, inapaswa kuwa na jukumu la ushauri tu, Reuters imeripoti.
Elon Musk amesema hadharani kwamba anakubaliana na agizo la Trump. Kulingana na Politico, idara inayoongozwa na Musk ilikiri kuwa "ilifanya makosa kadhaa."
Chanzo: BBC Swahili
Nilisema na narudia kusema kuwa, urafiki wao hautadumu mpaka mwisho wa muhura wa Trump.
Elon Musk ni mjanja mjanja opportunist tu na pale anapoona hakuna maslahi binafsi basi ananuna na kuanzisha vita.
 
Nilisema na narudia kusema kuwa, urafiki wao hautadumu mpaka mwisho wa muhura wa Trump.
Elon Musk ni mjanja mjanja opportunist tu na pale anapoona hakuna maslahi binafsi basi ananuna na kuanzisha vita.
Ngoja tuone muda utaongea.
 
Dingi= Mzee wa Mawigi
1000096207.jpg
 
Inch ya Marekani inaongozwa kwa logic ya k-private sector.

Ukileta bong hiyo logic
Tunaweza hoji tija ya kwa nini kwenye wilaya kuwe na DED halafu kuna DC na DAS. Halafu kwa nini tuwe na Katibu tarafa wakati kuna Mtendaji wa kata.

Ningedhani kungekuwepo RC,RAS,DED,WEO ,VEO ,madiwani na wenyeti wa serikali ya mtaa au kijiji
 
Watu mnafurahisha sana mko so-overwhelmed with the American affairs kiasi kwamba mnasahau hata kwamba mko kwenye nchi nyingine ambayo iko hoi katika kila sekta na wala hakuna anayejali..😛😛😛
 
Sisi waturejeshee tu dawa za kuongeza maisha za UKIMWI laa sivyo tunaenda kuadhirika sana.
 
Back
Top Bottom