Trump aanza kuirudisha Marekani mahala pake, mwezi May aongeza ajira mpya 2.5M

Trump aanza kuirudisha Marekani mahala pake, mwezi May aongeza ajira mpya 2.5M

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Ndio maana mimi sio muumini wa hizi zinaitwa projections au utabiri kutoka kwa wataalamu au wachambuzi wa utabiri sijui analysts projects this, projects that. Mimi hua nasema hizi ni sawa na usoma nyota na upiga ramli.

Kwa mfano wanaoitwa wataalamu wa uchambuzi walitabiri Afrika tutakua na vifo 100,000 kwa mwezi April hadi May, cha ajabu hata vifo 10,000 hatujafikia.

Sasa wachambuzi walitabiri Mwezi May Marekani itapoteza ajira rasmi milioni 8 kutoka milioni 15 zilizopotea mwezi April sababu ya lockdown. Mwezi March ajira milion 5 zilipotea.

Toka covid-19 imeanza ukosefu wa ajira Marekani umeongezeka kwa 9.8% hadi 17.5% maana ulikua chini ya 10% toka Trump aingie madarakani. Watabiri wakasema kufikia May kutakua na ukosefu wa ajira wa 20% .

Ajabu ni kua Trump amewashinda wataalamu wa itabiri na usoma nyota, mwezi May ameongeza ajira 2.5M na zinategemea kuanza kuongezeka. Inawezekana kabisa kufikia October Trump akawa amerudisha ajira zote zilizopotea kipindi cha corona.

Trump mwenyewe husema kwa records hakuna rais anaemfikia katika historia ya Marekani isipokua Abraham Lincoln tu. Ukweli hili halina ubishi, records speak for themselves. Trump has done it all.

Baada ya corona Joe Biden alianza kupata mvuto na kumpita Trump kwa zile tabiri au ramli za mitandaoni ambazo hata hivyo hazijawahi kumbeba Trump toka anaanza kampeni 2016. Trump always beats the analysts, projections.

Trump hails jobs numbers and "equality," says it's a "great day" for Floyd Trump hails jobs numbers and "equality," says it's a "great day" for Floyd

U.S. labor market unexpectedly improves; recovery years away
 
Mahaba niue! Kama unaamini kila anachosema Trump .... sijui jinsi ya kumalizia. Anajisema yeye ni genius. Magenius wote tunaowajua wa sayansi, teknolojia, teknohama, sanaa, fasihi, nk hawajisemi. Lakini wewe utamwamini anayejitangaza kwamba ni genius!!!🙄🙄🙄🙄🙄🙄
 
Trump hasemi records ndizo zinasema.

Ndio maana Dems wanategemea corona kumuangusha Trump ila vinginevyo hawana chochote au hoja ya kupambana na Trump. Bilionea Michael Bloomberg alisema kwa hali iliyopo Democratic hawana mtu wala hoja ya kupambana na Trump.

Hapa sio mahaba ni statistics.
 
Trumpets mna kazi sana, hizo kazi zimepngezekaje wakati watu wako ndani?
 
Hajasema Trump. Muwe mnatafuta taarfa
Mahaba niue! Kama unaamini kila anachosema Trump .... sijui jinsi ya kumalizia. Anajisema yeye ni genius. Magenius wote tunaowajua wa sayansi, teknolojia, teknohama, sanaa, fasihi, nk hawajisemi. Lakini wewe utamwamini anayejitangaza kwamba ni genius!!![emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Mahaba niue! Kama unaamini kila anachosema Trump .... sijui jinsi ya kumalizia. Anajisema yeye ni genius. Magenius wote tunaowajua wa sayansi, teknolojia, teknohama, sanaa, fasihi, nk hawajisemi. Lakini wewe utamwamini anayejitangaza kwamba ni genius!!!🙄🙄🙄🙄🙄🙄
Kwa akili yako Trump anaweza ku-fake data kwenye Democratic and transparency country kama hii?
.
Tanzania Magufuli akisema kaajiri watu 10 hata kama hajaajiri hata mmoja itakuwa hivyo sasa pinga uone
 
Trumpets mna kazi sana, hizo kazi zimepngezekaje wakati watu wako ndani?
Ndani ya wapi?
america hakuna lockdown kuna curfew tu baadhi ya miji huku including mji naoishi
 
Trump hasemi records ndizo zinasema.

Ndio maana Dems wanategemea corona kumuangusha Trump ila vinginevyo hawana chochote au hoja ya kupambana na Trump. Bilionea Michael Bloomberg alisema kwa hali iliyopo Democratic hawana mtu wala hoja ya kupambana na Trump.

Hapa sio mahaba ni statistics.
Jamaa walitaka sana aweke lockdown uchumi uanguke waitumie kama silaha yao November.
 
Mahaba niue! Kama unaamini kila anachosema Trump .... sijui jinsi ya kumalizia. Anajisema yeye ni genius. Magenius wote tunaowajua wa sayansi, teknolojia, teknohama, sanaa, fasihi, nk hawajisemi. Lakini wewe utamwamini anayejitangaza kwamba ni genius!!![emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
Nami nasema Trump ni Genius, ndiyoo, Ni genius wa uongozi na uchumi.
 
Trump ni Akili kubwa ila wajinga wajinga ndo walishashindwaga kabisa kumuelewa.
 
Trump namkubali lakini Kama yuko too aggressive kwenye foreign policy na yule secretary wake Pompeo, Hawa wanaweza sababisha cold war nyingine na China, kitu ambacho sio kizuri kwa yoyote
 
Trump namkubali lakini Kama yyoo too aggressive kwenye foreign policy na yule secretary wake Pompeo, Hawa wanaweza sababisha cold war nyingine na China, kitu ambacho sio kizuri kwa yoyote
China ime-take advantage ya udhaifu wa viongozi wa Marekani muda mrefu sana ndio maana imefikia hapo.

Sasa Trump anaziba ile mianya ambayo China ameitumia kufaidika kwa muda mrefu.

Trump anasema isingekua udhaifu wa viongozi wa Marekani China isingefika hapo.

Records zinambeba Trump, hana masihala. China ni washenzi sana usipowakazia hawan huruma.
 
Jamaa walitaka sana aweke lockdown uchumi uanguke waitumie kama silaha yao November.
Wasenge kina mavi ccn na mabilionea uchwara wa Marekani ambao walikua wakipata tender za kifisadi za shauri sijui ujinga gani, tuwanyonya wamarekani Trump ameimgia amekata hiyo mizizi hawampendi.

Trump anasema anafanya kitu kinaitwa drain the swamp. Watu walikua wanaacha kazi walizoajiriwa nazo serikalini wanafungua vikampuni uchwara vya ushauri kwa kazi ile ile walioacha na kucheza janja janja na kupiga hela. Trump ametunga sheria ya kuzuia hiyo janja janja, watu kama hao watampenda kweli? Ndio wanaoitwa cnn kila siku kutoamaoni negative dhidi ya Trump.

Makampuni ya vifaavya ulinzi yalikua yanaiuzia Marekani vifaa kwa bei ghali sana na ku-inlate thamani ya vifaa Trump akakataa.

Benzon amekua akitumia postal service za Marekani lakini eti bado postal service ndio wanamlipa yeye kutumia service zao. Teump akasema hii ni akili au bangi.

Matajiri wengi ambao wametumia miaka na miaka kuwanyonya wamarekani na vybo vyao vya habari hawawezi kumpenda Trump.
 
China ukiizembea wanakuumiza. Pompeo na Trump are the right people. Pata picha Pompeo angekuwa VP
Trump namkubali lakini Kama yyoo too aggressive kwenye foreign policy na yule secretary wake Pompeo, Hawa wanaweza sababisha cold war nyingine na China, kitu ambacho sio kizuri kwa yoyote
 
Wasenge kina mavi ccn na mabilionea uchwara wa Marekani ambao walikua wakipata tender za kifisadi za shauri sijui ujinga gani, tuwanyonya wamarekani Trump ameimgia amekata hiyo mizizi hawampendi.

Trump anasema anafanya kitu kinaitwa drain the swamp. Watu walikua wanaacha kazi walizoajiriwa nazo serikalini wanafungua vikampuni uchwara vya ushauri kwa kazi ile ile walioacha na kucheza janja janja na kupiga hela. Trump ametunga sheria ya kuzuia hiyo janja janja, watu kama hao watampenda kweli? Ndio wanaoitwa cnn kila siku kutoamaoni negative dhidi ya Trump.

Makampuni ya vifaavya ulinzi yalikua yanaiuzia Marekani vifaa kwa bei ghali sana na ku-inlate thamani ya vifaa Trump akakataa.

Benzon amekua akitumia postal service za Marekani lakini eti bado postal service ndio wanamlipa yeye kutumia service zao. Teump akasema hii ni akili au bangi.

Matajiri wengi ambao wametumia miaka na miaka kuwanyonya wamarekani na vybo vyao vya habari hawawezi kumpenda Trump.
Trump na CNN kwani Ni ishu ya ufisadi au.
Ni itikadi? Trump yupo too conservative wakati CNN wapo too liberal, actually sio CNN tu, vyombo vingi vya habari vimeegemea upande wa Liberals, hata Ulaya media nyingi zipi liberal mf BBC, DW

Yaani Trump kidogo awe kwenye kundi moja na wale radicals wa Far Right
 
Kusema ukweli Trump ndio Rais ambaye ameweza kusimamisha mbinu zote za China kutaka kuipiku Marekani, China na kelele zote kuwa uchumi wake ungeenda kuipita Marekani lakini kwa akili finyu wakitegemea kuuza bidhaa zao Marekani, ndio maana china kaanzisha hiki kirus ili kumdhoofisha Marekani lakini ni kama kachochea moto maana nchi nyingi duniani zimechukia sana marekani alivyopata janga kwa ukubwa maana ndio soko lao.

China alikuwa anauza more than 600 billion per year na Marekani aliuza just 130bln per year katika balance of trade means China side alikuwa anapata faida ya (600-130)= +470 while America ilikuwa inapata loss of -470 every year. Sasa Trump kawaonya China kuwa anataka 0 Import from China na wanalilia tu na kujifanya ni wababe lakini hamna nyota wataacha kuona.

Kuna mpango wa chini chini ambao unaendeshwa na Marekani wa kushawishi nchi zote zenye makampuni china kuyaondoa, sasa hiyo sijui itakuweje maana hiyo itakuwa pigo takatifu. Na nchi nyingi mfano Japan imeshaanza ketenga budget ya kuondoa makampuni yake china, na nyingine nyingi tu.

Kuna mengi ya kumsifu Trump na tunampa pongezi nyingi sana aendelee kukaza uzi
 
Back
Top Bottom