Trump abadilisha jina la Hormuz na kuwa Strait of Trump

Trump abadilisha jina la Hormuz na kuwa Strait of Trump

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Marekani Donald Trump amechapisha ramani kwenye mtandao wake wa kijamii Truth Social ikionyesha Strait of Hormuz ikiwa imepewa jina la “Strait of Trump,” badala ya jina lake rasmi la Strait of Hormuz, maarufu Mlango Bahari wa Hormuz.

Mlango huo wa bahari ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za usafirishaji wa mafuta duniani, huku mgogoro wa Marekani na Iran ukiwa bado unaendelea.

Wachambuzi wamelitafsiri tukio hilo kama ujumbe wa kisiasa au wa kuamsha mjadala, unaoendana na mtindo wa Trump wa kutumia kauli zenye mvuto mkubwa wakati wa hali za mvutano wa kisiasa.

Hii si mara ya kwanza Trump kwa kutoa kauli kama hiyo. Katika taarifa ya awali, alionekana kuchanganya jina hilo, akisema Iran inahitaji "kufungua Mlango wa Trump, hapo hapo akaghairi na kusema kuwa alimaanisha Hormuz."

1777550462369.png

1777550498963.png
 
Trump ndio rais wa kwanza duniani ambaye anabadilisha maneno , vita alivyoshindwa anasema yeye kashinda, Mlango wa bahari upo chini ya IRGC Iran yeye anasema upo chini yake, anasema Iran kaidhoofisha lakini Teheran wanasherehekea na kufurahi leo siku ya 60 na kulipongeza jeshi lao kwa ushindi mkubwa wa historia, Iran juzi ilifungua kiwanja chake cha ndege toka vita kusimama shughuli zinakwenda kama kawaida,

Nafkiri Trump akili zake haziko sawa lakini kama ziko sawa hem aulizwe maswali haya yafuatayo atajibu nini:-
1. Alisema anataka oil ya Iran je amepata?
2. Alisema yeye shida yake ni Kharg island kisiwa cha mkakati je amekipata?
3. Alisema anataka madini ya Urenium yaliyoyushwa na Iran apewe yeye je amepewa?
4. Alisema lengo hasa la vita ni regime change je alifanikiwa kubadilisha huo utawala na kuekwa wa kwake
5. Na hili la nuclear alisema ataizuia Iran isitengeneze silaha ivi ameweza? Iran wamejifungia huko ata hajui wana nini au wanya nini na pengine iran mzigo wa Nuclear anao wa kutosha.
6. Alisema Iran atahakikisha inarudi zama za Stone Age hivi Iran imerudi huko?

Na mengine mengi sana, ni kama vile fedha za walipa kodi wa marekani ameenda kuzimwaga bahari dola bilioni 25 walizokiri jana kwamba zimetumika kwenye hiyo waitayo vita bila ya mafanikio.
 
Trump anamfanya George W. Bush aonekane saint
 
Kwa Mara ya kwanza USA wameongozwa na mtu mjinga mshamba na limbukeni
Nadhani kina Obama Huwa wanachekea chooni

Pressdar anawezaje kufanya ujinga kama huo , hivi Hana washauri !? Au ndio amezungukwa na machawa !?
 
Trump ana akili nying sana huyu Rais, acheni tu hormuz iitwe Trump
 
Wenye akili nyingi ndio tunaomuelewa Trump anachofanya
 
Huyu mzee ndivyo alivyo nashangaa waliomchagua kwenye hiyo nafasi.

Hana tofauti na Lisu wa Chadema, akili zao zinafanana.
 
Back
Top Bottom