Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mgombea mtarajiwa wa kiti cha uraisi wa Marekani na pia mshtakiwa aletiwa hatiani kwa makosa ya kughushi nyaraka Donald Trump leo ameongea na waandishi wa habari na wafuasi wake katika ofisi zake mjini New York.
Akiongea kwa muda wa dakika zipatazo 40 kuashiria kila kosa alotiwa hatiani kwa makosa yote 34, bwana Trump ametumia muda mwingi kuwashambulia jaji aliesimamia kesi yake na wazee wote wa baraza ambao wamemkuta ana hatia ya kughushi nyaraka za hesabuzake za kulipa kodi.
Bwana Trump atarajiwa kutangazwa kuwa mgmbea uraisi wa chama cha Republican siku mbili baada ya hukumu kutolewa mwezi Julai.
Lakini leo mchana akiongea na wafuasi wae na waandishi wa habari katika jumba lake maarufu kama Trump Tower, bwana Trump ametoa madai ya kuamsha akili pale alipodai kwamba kuna wafungwa kutoka Congo DRC Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao wamekuwa wakipelekwa Marekani bila kufafanua kwamba wafungwa hao wapelewa huko kwa makusudio yepi.
Wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya Afrika na huko Congo DRC harakaharaka wamekanusha madai hayo ya Donald Trump na kusema madai hayo hayana ukweli wowote.
Serikali ya Congo DRC pia imekanusha kuwepo kwa zoezi hilo ambalo kama lipo ni la kustaajabisha.
Je, ni kweli wapo wafungwa hawa wanopelekwa huko Marekani na kwa malengo yepi?
Au ndo kupewa mafunzo ya kijeshi kwa ajili ya kutumika kuleee...