Trump afutiwa kesi ya kuingilia matokeo ya uchaguzi 2020

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ameondolewa mashtaka yaliyokuwa yakimkabili, wakati akielekea kuapishwa kama rais wa 47 wa Marekani Januari 20, 2025.

Kulingana na kituo cha VOA, Jaji wa Mahakama ya Washington, Tanya Chutkan Jumatatu aliondoa mashtaka ya kuingilia matokeo ya uchaguzi wa rais wa 2020 dhidi ya Trump.

Hatua hiyo ni kufuatia ushauri kutoka kwa mwendesha mashtaka maalum wa Marekani, Jack Smith aliyewasilisha waraka Mahakamani, kwamba sera ya muda mrefu ya idara ya Mahakama inaondoa mashitaka dhidi ya Rais aliyeko madarakani.

Pia soma:
- Baada ya Donald Trump kushinda uchaguzi wa urais Marekani kesi mbili zake zitaendelea Mahakani?

Kwenye ombi lingine kwa Mahakama, Smith ameiomba Mahakama ya rufaa ya Atlanta imuondoe Trump kwenye kesi ya rufaa iliyokuwa inasubiriwa. Waendesha mashtaka wa Atlanta awali waliwasilisha rufaa ya kutaka Trump aendelee na kesi ya tuhuma za kupatikana na nyaraka muhimu za serikali kwenye nyumba yake ya Florida baada ya kuondoka madarakani 2021.

Trump kupitia mtandao wa Truth Social amesema kuwa kesi hizo pamoja na nyingine nyingi zililazimishwa na wala hazina msingi wowote na wala hazikufaa kuwepo kamwe, huku akieleza kuwa chama cha Demokratiki kimetumia zaidi ya dola milioni 100 za walipa kodi, kupitia kesi dhidi yake kama mpinzani wao wa kisiasa.
 
hongera sana dumeee, mwamba trump mazee uko vizuriii....unaingia kambini kutusafishia makobazi...yatanyookaa
 
Ingekua ni nchi Fulani Africa Mashariki, wanalalamika hao, ungeskia mahakama haiko Huru, dah 🐒
 
Huko chama tawala hakikutumia dola wala mawakala ili kibaki madarakani na mpinzani baada ya kushinda akatangazwa. Sasa vipi nchini kwako unaweza kuyafanya hayo? Jibu ukweli japo kiunafiki tu.
 
Ila chama tawala kimefuta kesi right?

najaribu kufikiria risasi ya skio ingesemwa nini Tz, dah!

Mungu anajua sana aise 🐒
 
Back
Top Bottom