Trump amechomoa betri ghafla, serikali za Afrika zenye viongozi walioshindwa kutumia rasilimali za nchi zao hawajui nini wafanye

Watatubana kwenye kodi
Na wewe utakubari umeme unazalishwa Nchini kwako kwenye ardhi ya Nchi yako mfano wewe wa Tunduma unauziwa unit 1 kwa 400/= halafu mtu wa Zambia Lusaka anauziwa unit 1 kwa 150/= halafu unachekelea wanatubana kwenye kodi
 
Ila hiyo executive order ya Trump imepelekwa Mahakamani,sidhani kama itafanya kazi.
Itafanya kazi na namiombea Mungu ifanye kazi

Najua iliyopelekwa ni kuhusu uraia wa kuzaliwa ,watt wanaozaliwa kule kuwa raia..
 
Trump anawajua viongozi wa Afrika kuliko hata sisi waafrika tunavyowajua viongozi wetu. Haya maamuzi anayoyachukua Trump ni kwa manufaa ya waafrika.
Kaona trip nyingi za viongozi wakubwa kwenye nchi za mbali, wakitumia madege makubwa huku yamebeba watu kibao.
 
Mtu anajinyima rasilimali zake anakupa wewe, badala ya kutumia kwa manufaa ya watu wako;
1. Unanunua magoli kwa 5m?
2. Unanunua Sa100 2025 pikipiki nchi nzima?
3. Unanunua zaidi ya mabasi 200 ya ccm?
4. Unapeleka wajumbe zaidi ya 1,000 Dodoma na kuwapa more than 2m? Ili tu wakupitishe bila kuzingatia demokrasia?

Mwenzako anawakamua matajiri na watu wake kodi kubwa ili akupe wewe.
 
Trump asifiwe kwa ubunifu uliotukuka, tunapewa misaada kisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anasema tunatibiwa kwa dawa za mama! Wajinga wanampigia makofi! Humu wamejaa tele akina Lucas Mwashambwa.
 
Trump asifiwe kwa ubunifu uliotukuka, tunapewa misaada kisha mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam anasema tunatibiwa kwa dawa za mama! Wajinga wanampigia makofi! Humu wamejaa tele akina Lucas Mwashambwa.
Akina Luca na rafiki zao kama ni wasomi wa nchi hii yafaa wakamatwe warudishwe kusoma chekechea kwa lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…