Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hapa ndipo vita vilipofikia.
Baada ya askari wa Ukraine walioingia eneo la Kursk mwaka jana kuzingirwa na kuwa karibu na kifo,raisi wa Marekani amewaombea huruma askari hao kutoka kwa raisi wa Urusi
Akiandika kwenye mtandao wake wa Truth ,Trump amemuomba Putin awaache askari hao warudi kwao wakiwa hai.
Tamko hilo la Trump linafuatia lile la Putin ambaye baada ya kuthibitisha kukombolewa eneo la Kursk na kuzingirwa kwa askari hao miongoni mwa askari bora waliobaki wa Ukraine,alisema wapiganaji hao ama wajisalimishe au watauwawa wote.
Hatua hiyo ya Trump pia inafuatia malalamiko ya raisi Zelensky wa Ukrain akisema kila siku iendayo na maisha yanapotea.Kwa maneno hayo akamuomba Trump asaidie kuokoa maisha hayo.