Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Uchaguzi unaoendelea huko Marekani umeonyesha kila aina ya rangi. Wakati wagombea wote wakichuana vikali, na huku ikionekana kuwa kura za waislamu na waarabu katika swing states kama vile michigan zinaweza kuamua nani awe mshindi wa kinyang'anyiro hicho.
Wagombea wote "rhetorically" wanaonekana hakuna hata mmoja aliyeahidi kubadili policy ya USA kuwa unconditional supporter wa Israel. Kamala Harris yeye amesema Biden anafanya kazi nzuri na hatabadili chochote cha Biden, wakati Trump yeye akisikika kumshauri Netanyahu kuwa anafanya kazi "nzuri" na amalizie kazi huko Gaza "Finish the Job".
Hata hivyo nyakati nyingine kauli za wanasiasa majukwaani wakati wa kuomba kura siyo ambazo viongozi hao huziweka ktk matendo wakishaapishwa, kwa mfano Trump alikuwa na slogan ya "lock her up", yaani kumtia ndani Hillary Clinton pindi akipata urais takriban miaka 8 iliyopita, lakini alivyopata urais hakumfunga. Trump pia alikuwa ananadi kujenga ukuta ktk mpaka na mexico lakini alivyoupata urais hakufanya hilo. Kwa hiyo hata hizi kauli za Trump za kujifanya anamchagiza Netanyahu "kufinish job" huko Gaza huenda ni maneno ya kutafuta kura za "Evangelicals" wa marekani na mahela ya Zionists.
Ila Trump anamuelewa vizuri Netanyahu kuwa ni mtu asiyetaka amani. Trump amewahi kunukuliwa akisema kuwa mwanzoni nilidhani Netanyahu ni mtu wa amani na kwamba wapalestina ndiyo wanaokwamisha jitihada za amani baadae nikagundua kuwa Netanyahu ndiye mkwamishaji mkuu wa amani.
Trump pia ana mkwe wa kiarabu. Binti yake aitwaye Tiffany kaolewa na Mlebanoni, Naamini kabisa hii itakuwa na influence ya maamuzi ya Trump kusapoti Israel kuwapiga wakwe zake au kuingilia kati na kuzuia. Labda ndiyo maana Israel sasa hivi imejiweka katika posture ya kutaka kuwind up operation ya Lebanoni fasta kabla Trump hajaapishwa.
Kwa wachambuzi wa kisiasa, ni dhahiri Trump akishaingia madarakani itakuwa ni vigumu sana kwa mazionists kumcontrol. Jamaa kashinda vita nyingi mno walizomuwekea kama vikwazo asivuke, walimuimpeach, wakafeli, wakamfungulia kesi, wakaangukia pua, wakajaribu kumuua wakafeli. Ukizingatia hii term ni term yake ya mwisho na hatoomba kura tena basi hana cha kuogopa pindi akishapata. Ndiyo maana huenda Trump akaja kugeuka shubiri kwa Mazayuni.