Trump anaandaa Mazingira ya kupeleka jeshi la Mapigano nchini Ukraine dhidi ya Urusi?

Kwenye hili game pale Ulaya Urusi anawaacha wanakaa vikao vyao weeeh, mwisho wakimaliza anaanzia pale walikoishia.

Ni jeshi lipi lipo tayari kwenda kukaa kwenye ardhi ya Ukraine likisimama dhidi ya Urusi kwa kisingizio chochote?
Urusi inaposema Ukraine isijiunge NATO sio kwamba Marekani na washirika wake wanashindwa kuiunga kwa nguvu bali shida inakuja wakishaiunga ikawa mwanachama wao itahitajika jeshi kwenda kumlinda mwanachama wao mpya.

Nato wanaweza kufanya jambo kama hili? Jibu ni haiwezekani hata kidogo sababu itakuwa ni tangazo la moja kwa moja la vita dhidi ya Urusi.
Hata sasa usione rais wa Ukraine alivyokubali haraka kumwachia Marekani rasilimali zake ukadhani ni mjinga, hapana. Anajua ili Marekani achume hizo rasilimali itampasa apeleke jeshi kitu ambacho kitakuwa ni kama ameungwa NATO.
Kinachoenda kutokea Marekani itasaini mkataba alafu ije kusaini mkataba mwingine na Urusi wa kuifanya Ukraine nchi isiyokuwa na jeshi bali usalama wa nchi ya Ukraine utakuwa mikononi mwa Urusi.

Kwa kifupi ili Marekani aweze kupata anachokitaka pale Ukraine ni lazima Ukraine isalimishwe chini ya miguu ya Urusi... Nje ya hapo basi vita vitaendelea hadi vipelekee vita vya dunia kwa sababu UKRAINE ni roho ya Urusi kama wenyewe wasemavyo. Haihitaji mjadala mkubwa maana kila kitu kipo wazi ndio maana hata rais mpya wa Marekani anayasema waziwazi.
Kama nakuelewa mkuu. Naona Sasa Eu and particularly France and Uk wanataka nao wapewe madini ya Ukraine. Trump ni Genius like Putin
 
Nani alilitoa Morali maana kwa miaka kadhaa Jeshi Hilo Hilo lilimzuia Tai kufika Damascus
Safari hii ya mwisho mpaka kutokea mapinduzi halikuwa na morale, uliona mwenyewe waasi walikuwa tu wanajichukulia miji mpaka wanafika Damascus. Hakukuwa na resistance ya maana
 
Kama nakuelewa mkuu. Naona Sasa Eu and particularly France and Uk wanataka nao wapewe madini ya Ukraine. Trump ni Genius like Putin
Ndio maana yake japo Trump anaona kama mgao utapungua.
Tuwe tu watazamaji sababu maamuzi ya mwisho yatatoka Kremlin... Magharibi wameambiwa kwenye maswala ya kijeshi wasahau kabisa pale Ukraine ila kwenye mambo ya kiuchumi ndipo wameambiwa watajua wao ila serikali mjini Kiev ni lazima iwe tiifu chini ya Urusi, na hiki ndicho kitamtosa zelensky sababu yeye anataka jeshi wakati bwanaake Marekani anajua kupeleka jeshi ni kama kwenda kudumbukia kwenye tanuru la moto na maslahi yake hayatatekelezeka.
Hivyo itatakiwa aondoke madarakani atafutwe mtu atakaekubali kuwa chini ya Urusi ndipo Marekani ichimbe madini huku ikiijenga Ukraine iliyosalimishwa Moscow
 
Watu wengine mnapoandika sijui mnavuta bange, vita vya ghuba alivyosaidiwa Iraq na Marekan havikuwa na changamoto kubwa khs usalama wa Marekan, lkn direct war kati ya Urusi na Marekan kwa kisingizio tu cha kupata Maadini yaliyokuwepo Ukraine hilo halitowezekana, sio kipindi kile cha Biden wala wkt huu wa Trump. Tuweni serious jamani
Tunakuwelewa wachache tunaofatilia mambo bila ushabiki.
Direct confrontation (war) kati ya urusi na marekani hatakuja kutokea. Hawa wakubwa wa dunia wanajuana uwezo wao
 
Kwenye hili game pale Ulaya Urusi anawaacha wanakaa vikao vyao weeeh, mwisho wakimaliza anaanzia pale walikoishia.

Ni jeshi lipi lipo tayari kwenda kukaa kwenye ardhi ya Ukraine likisimama dhidi ya Urusi kwa kisingizio chochote?
Urusi inaposema Ukraine isijiunge NATO sio kwamba Marekani na washirika wake wanashindwa kuiunga kwa nguvu bali shida inakuja wakishaiunga ikawa mwanachama wao itahitajika jeshi kwenda kumlinda mwanachama wao mpya.

Nato wanaweza kufanya jambo kama hili? Jibu ni haiwezekani hata kidogo sababu itakuwa ni tangazo la moja kwa moja la vita dhidi ya Urusi.
Hata sasa usione rais wa Ukraine alivyokubali haraka kumwachia Marekani rasilimali zake ukadhani ni mjinga, hapana. Anajua ili Marekani achume hizo rasilimali itampasa apeleke jeshi kitu ambacho kitakuwa ni kama ameungwa NATO.
Kinachoenda kutokea Marekani itasaini mkataba alafu ije kusaini mkataba mwingine na Urusi wa kuifanya Ukraine nchi isiyokuwa na jeshi bali usalama wa nchi ya Ukraine utakuwa mikononi mwa Urusi.

Kwa kifupi ili Marekani aweze kupata anachokitaka pale Ukraine ni lazima Ukraine isalimishwe chini ya miguu ya Urusi... Nje ya hapo basi vita vitaendelea hadi vipelekee vita vya dunia kwa sababu UKRAINE ni roho ya Urusi kama wenyewe wasemavyo. Haihitaji mjadala mkubwa maana kila kitu kipo wazi ndio maana hata rais mpya wa Marekani anayasema waziwazi.
Umeeleza vizuri sana, umenipanua ufahamu
 
Ndio maana yake japo Trump anaona kama mgao utapungua.
Tuwe tu watazamaji sababu maamuzi ya mwisho yatatoka Kremlin... Magharibi wameambiwa kwenye maswala ya kijeshi wasahau kabisa pale Ukraine ila kwenye mambo ya kiuchumi ndipo wameambiwa watajua wao ila serikali mjini Kiev ni lazima iwe tiifu chini ya Urusi, na hiki ndicho kitamtosa zelensky sababu yeye anataka jeshi wakati bwanaake Marekani anajua kupeleka jeshi ni kama kwenda kudumbukia kwenye tanuru la moto na maslahi yake hayatatekelezeka.
Hivyo itatakiwa aondoke madarakani atafutwe mtu atakaekubali kuwa chini ya Urusi ndipo Marekani ichimbe madini huku ikiijenga Ukraine iliyosalimishwa Moscow
Mkuu sasa umenishawishi mazima kuamini unachosema
 
Safari hii ya mwisho mpaka kutokea mapinduzi halikuwa na morale, uliona mwenyewe waasi walikuwa tu wanajichukulia miji mpaka wanafika Damascus. Hakukuwa na resistance ya maana
Saw shida ya mrusi huwa anazubaa sana ndo maana Marekani aliisambaratisha soviet union (USSR) mpaka ikabaki vipande vipande
 
Hivi karibuni kumekuwa na majibishano makali kati Kyiv na Washington juu ya mpango wa kuleta Amani nchini Ukaraine,Rais wa Ukraine Mr Zelensk akiishutumu Washington juu ya kujihusisha katika mazungunzo na Urusi juu amani ya Ukraine pasipo kujumuishwa wao Ukraine amabao ni wathilika wakubwa

Kama hiyo haitoshi wakaingia katika mabishano mengine juu ya mkataba wa madini adimu yanayopatikana Ukaraine, Washington chini ya raisi Trump wanataka madini hayo yatumike kugharimia vita lkn Kiev ilikataa awali lkn baadaye inaonekana kukubali na hapa ndo nataka kuzungumzia

Jambo hili la kukubali kwa Kiev kutia Saini na marekani juu ya madini yake kunaiweka Ukarine miongoni mwa mataifa yenye Maslahi ya moja Kwa Moja ya Marekani

Sheria ya Marekani ya sasa itamruhusu raisi Tramp baada kukamilika kwa mkataba huo kuruhusu jeshi la nchi hiyo kuingia kupigana Moja Kwa Moja nchi Ukraine kulinda Maslahi ya Marekani

Sheria hii imewahitumika katika vita vya ghuba pale Iraq ilipoivamia Kuwait mnamo miaka ya 90s kwa sababu Narekani ilikuwa na maslahi ya Moja kwa Moja nchini humo katika swala la Mafuta

Sheria hiyo pia inaweza tumika nchini Uchina iwapo China itaivamia Taiwan maana Taiwan inamaslahi ya Moja kwa Moja ya Marekani katika swala teknolojia ya chip .Na swala la majeshi ya marekani kupelekwa taiwani lilithibitishwa na Rais wa marekani aliyepita Joe baiden

Hivyo Putini anatambua vilivyo Nia ya Marekani juu ya mkataba huu wa madini hebu tuone kitakachoendelea
Food for war
 
Safari hii ya mwisho mpaka kutokea mapinduzi halikuwa na morale, uliona mwenyewe waasi walikuwa tu wanajichukulia miji mpaka wanafika Damascus. Hakukuwa na resistance ya maana
Hii ya Congo inataka kufanana na ya Syria
 
Back
Top Bottom