SI KWELI Trump anasema anaweza kuwapoteza wakatoliki na ana mafaili yao

SI KWELI Trump anasema anaweza kuwapoteza wakatoliki na ana mafaili yao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nyie si mnajifanyanga sijui katoliki inaongoza dunia
Haya Trump amesema anaweza kulizimisha kanisa lote na kulipoteza
Vatican files hizo utakuta ndio mambo yote ya kulawiti watoto dunia nzima

Trump wakatoliki.jpg
 
Tunachokijua
Kumekuwepo na 'screenshot' kutokea mtandao wa Truth social ikiwa na utambulisho wa Rais wa Marekani Donald Trump, huku ikiwa na ujumbe unaodaiwa kutolewa na Rais huyo ukisomeka;

"Kama Rais wa Marekani, nina uwezo wa kupata taarifa ambazo zinaweza kuiangusha Upapa, Vatican na Kanisa lote Katoliki kwa muda mfupi sana! Hizi zinaitwa mafaili ya Vatican, ambayo sitayatoa kwa heshima ya Wakatoliki bilioni moja duniani kote.

Hata hivyo, Papa dhaifu wa Vatican, Leo, anapaswa kukumbuka ni kwa nani anapaswa kuwajibika ikiwa ataendelea kuingilia siasa kwa niaba ya utawala unaoitwa wa kigaidi wa Iran. Upotoshaji anaousambaza Papa kuhusu operesheni maalum ya kijeshi ni hatari sana.

YESU angependa AMANI KUPITIA NGUVU, kama ninavyofanya! Iran haitawahi kuwa na silaha za nyuklia, na tutatumia NGUVU zetu KUBWA kuhakikisha hilo halitokei! Hii ndiyo NJIA YA AMANI. Asanteni kwa kunisikiliza kuhusu suala hili! – Rais DJT"


Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa nukuu hiyo ni ya kughushi na haijatolewa na Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake huo.

Kupitia utafutaji wa maneno muhimu katika ukurasa rasmi wa Truth social wa Rais Donald Trump hakuna kumbukumbu kuonesha kuwa alichapisha ujumbe huo Aprili 16, 2026.

Ujumbe uliopo kwenye ukurasa wake ni wa Aprili 13, 2026 ambapo Rais Trump alimuita Papa Leo XIV ni dhaifu na kwamba aliweka kwenye nafasi hiyo ili kumdhibiti. Haya yalijiri kipindi ambacho vita kati ya Marekani, Iran na Israel ikiendelea na hivyo Papa kupinga vikali hatua ya Marekani kuishambulia Iran.
For sure, The next President is Kamara Harris.

Tujaribu kuwapa wanawake nafas kubwa za uamuzi na ushawishi wa kisiasa kwenye hii dunia.
 
Umesahau kuedit tarehe, hiyo tweet hapo inaonyesha ni tarehe 16, leo ni tarehe 20.
Pamoja na hayo, tarehe 16 Trump hakuandika hiko kitu

Moderator Active hizi nyuzi za uzushi hazifai jf
kula chuma hiko, acha kuweweseka
Kwani wewe ni mtoa taarifa wa trump au ulokole unakusumbua

 
🤪🙆‍♂️🔥😊🔪🔪😃😊😆😆
 
Anaweza Donald Trump
Make America Great Again
 
Nyie si mnajifanyanga sijui katoliki inaongoza dunia
Haya Trump amesema anaweza kulizimisha kanisa lote na kulipoteza
Vatican files hizo utakuta ndio mambo yote ya kulawiti watoto dunia nzima


View attachment 3575671
Jaribuni kuwa na utambuzi wa fake news kabla ya ku-post vitu. Fanya utafiti kidogo juu ya ukweli wa vitu kama hivi kabla hujakimbilia ku-post.
 
Haya Trump amesema anaweza kulizimisha kanisa lote na kulipoteza
Vatican files hizo utakuta ndio mambo yote ya kulawiti watoto dunia nzima
Trump hana jipya hapo, anatapatapa tu ili asipingwe na kukosolewa juu ya Iran
 
Back
Top Bottom