Trump aogopa kupimwa Corona

Trump aogopa kupimwa Corona

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,104
Reaction score
6,827
Coronavirus: Sophie Gregoire Trudeau - mkewe waziri mkuu wa Canada akutwa na virusi

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na mke wake watabaki kwenye karantini kwa siku 14 , baada ya mkewe Sophie Gregoire Trudeau kukutwa na virusi vya corona.

Sophie Gregoire Trudeau ''anaendelea vizuri na dalili alizonazo si mbaya'' alisema mkurugenzi wa mawasiliano wa Waziri Mkuu.

Bwana Trudeau pia atakuwa kwenye karantini kama hatua ya tahadhari. Hatapimwa katika hatua za sasa kwa kuwa haoneshi dalili za maambukizi.

Katika ukurasa wa Twitter, Bi Sophie aliandika ''nitarejea nikiwa na afya njema hivi karibuni,''

Bi Trudeau amesema alikuwa amepata dalili ambazo hazikuwa za kawaida na kuongeza kuwa ''kuwa kwenye karantini si kitu ukilinganisha na familia nyingine nchini Canada wanaopitia haya''.

''Ninawatia moyo na kuwaweka kwenye fikra zangu (lakini zaidi tu ''nawatakia afya njema'' nawapatia pambaja kwa mbali!)'', alion

Image captiontrump

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hana mpango wowote wa kupima virusi, ingawa alikaribiana na afisa kutoka Brazil ambaye sasa amegundulika kuathirika na virusi hivyo.

Ikulu ya Marekani imesema hakuwa na mazungumzo na afisa huyo wa Brazil, hivyo hakukuwa na umuhimu wa kupima.

Fabio Wajngarten, Waziri wa mawasiliano wa rais wa Brazil Jair Bolsonaro, aliweka kwenye mtandao wa Instagram picha yake akiwa amesimama karibu na Rais Trump.
 
Babu (Trump) anaogopa vipimo? 😂😂😂
 
Anaogopa! kwani wanachoma sindano kupata specimen ya kupima korona?
 
Lazima aogope maana ni gonjwa pekee ambalo haliangalii una cheo gani linapiga kotekote😂
Tena wamuache tu anaweza amsha nyuklia zipambane na coro..😜
 
Kwa nini anaogopa ? Kwani wanachoma sindano? Au anaogopa vile wamesema wazee ndio waathirika zaidi Immune System iko low hivyo ukiupata swala la kurudi kwa muumba ni 70%
 
Dah Trump akipata Corona na age yake haponi, ataanza kukoroma na kuachia urais kiulaini😅
 
Trump pima hako kacorona tu.... Ni tumafua fulani twa kipumbavu tu.
 
Hapana, hatokuwa sahihi.

Hata mimi sina mpango wa kupima/ kupimwa.

Sijagoma kupima/ kupimwa.

Sina tu mpango wa kupima/ kupimwa.
Maybe uko sahihi.
Lakini kwa trump kutokuwa na mpango wa kupima ni ujinga coz hivi karibuni alikutana na ofisa wa kibrazili ambae amekutwa na ugonjwa huo.
Na Ivanka trump alikuwa na mkutano na ofisa wa australia ambae nae amekutwa na ugonjwa huo.
Kwa mtu mwenye kuchukua tahadhari angepima tuu.

Yasije yakamkuta ya Rudy Gobert
 
Back
Top Bottom