Trump apiga marufuku raia wa nchi 10 za Afrika kusafiri kwenda Marekani

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Trump apiga marufuku raia wa nchi 10 za Afrika kusafiri kwenda Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hatua hiyo inalenga kuwalinda Wamarekani dhidi ya vitisho vya usalama vya "kigeni".
Bara la Afrika ndilo bara lililoathiriwa zaidi na marufuku ya kusafiri iliyotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump, huku nchi saba kati ya 12 zikiwa kwenye orodha hiyo, itakayoanza kutekelezwa Jumatatu.

Amri hiyo inakataza watu kutoka Chad, Congo-Brazzaville, Equatorial Guinea, Eritrea, Libya, Somalia na Sudan - pamoja na Afghanistan, Myanmar, Haiti, Iran na Yemen - kuingia Marekani.

Aidha, kutakuwa na vikwazo vya usafiri kwa watu kutoka Burundi, Sierra Leone, Togo, Cuba, Laos, Turkmenistan na Venezuela - hawataweza tena kusafiri hadi Marekani kwa visa fulani.

"Hatutaruhusu watu kuingia katika nchi yetu ambao wanataka kutudhuru," Trump alisema kwenye video iliyowekwa kwenye X.

Chad wamefanya yanayotakiwa muda kwa wengine kusema nao pia.
 
Chad ni nchi moja ambayo hakuna mtu mwenye hamu ya kuitembelea hivyo kusema hawatatoa viza kwa wamarekani ni kujifurahisha tu.
 
Back
Top Bottom