The Zanzibar Echo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2025
- 490
- 838
Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Jumatano ametoa wito wa "kufutwa mara moja" kwa kesi ya ufisadi inayomkabili Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, ambayo ameitaja kuwa "haina umuhimu."
"Kesi inayomkabili mtu ambaye amejitolea sana, siwezi kufikiria kwangu. Anastahili bora zaidi kuliko hii. Kesi inayomkabili Bibi Netanyahu inapaswa KUFUTWA MARA MOJA," rais wa Marekani ameandika katika ujumbe mrefu uliochapishwa kwenye jukwaa lake la Truth Social.
Rais wa Marekani pia ametaja vita vya hivi majuzi vya siku 12 kati ya Iran na Israeli, ambapo Marekani ilishiriki pamoja na Israeli kwa kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran kabla ya kutangaza kusitisha mapigano kati ya pande hizo mbili. "Bibi Netanyahu amekuwa SHUJAA, kiongozi ambaye hajawahi kupatikana katika historia ya Israeli, na matokeo yake ni kitu ambacho hakuna mtu aliyefikiria kuwa kinawezekana: kutokomeza kabisa uwezekano wa kuwa moja ya nchi zenye silaha zenye nguvu zaidi za nyuklia ulimwenguni," Donald Trump amesema. "Pengine hakuna mtu ambaye angeweza kufanya kazi kwa maelewano bora zaidi na Rais wa Marekani kuliko Benjamin Netanyahu. Marekani iliiokoa Israeli (katika vita na Iran), na sasa Marekani itamuokoa Bibi Netanyahu."
Waziri mkuu wa Israeli anashitakiwa kwa hongo, ulaghai na uvunjaji wa uaminifu. Kesi yake ilianza mwezi Mei 2020 lakini ilikatizwa na vita katika Ukanda wa Gaza. Aliwasilisha maombi kadhaa ya kuahirishwa, akitaja uhasama uliochochewa na shambulio la vuguvugu la Kiislamu la Palestina Hamas dhidi ya Israeli mnamo Oktoba 7, 2023.
Benjamin Netanyahu ndiye waziri mkuu wa kwanza wa Israeli kukabiliwa na kesi ya jinai