Mpaka sasa njia ya kujifungia na kutokujifungia bado hazijaleta unafuu wa kuwa ndiyo njia ya kupunguza maambukizi ya Corona,
Hii ya kujifungia inanikumbusha Stori moja hivi ya wakoma, hawa watu walikimbia mjini na kwenda kujificha kuskojulikana Kwa sababu mjini mlikuwa na vita Kali Sana,
Wakoma hawa wakakaa huko ktk maisha ya dhiki kubwa, hapakuwa na chakula, mizizi na majani ndiyo ilikuwa ni chakula Chao huko
Siku moja walipoona njaa imewazidi Sana na miili Yao kuchoka taabani, wakakaa kushauriana, Jambo moja wakakubaliana kwamba, iwe mvua ama jua ni lazima twende mjini, mjini wakituu na watuuwe, maana hata tukibaki hapa bado tutakufa, mjini Kuna chakula, ya nini kubaki hapa tufe tunajiona?
Wakoma wakaamua Jambo moja, tunakwenda mjini ili kama ni kufa, tufe, kama tukibaki tutamshukuru Mungu,
Kumbe buana wale jamaa, katika tembea Yao Ile, Mungu aliweka mshindo mkubwa katika miguu Yao, kishindo kilichokuwa kinasikika ni kikubwa kiasi kwamba watu walio kilomita 10 Mbele, wanakisikia,
Watu wa mjini waliposkia hicho kishindo, walikimbia wakaacha kila kitu, silaha waluacha, madufulia ya chakula n.k
Basi ikawa ndiyo pona Yao hao jamaa,
Nataka kusemaje, Serikari zetu hizi zinazojaribu kujenga nchi zao ni za kiumaskini, kama serikali za nchi tajiri wanahofia uchumi Wao kuwafungia watu, hapa kwetu wakijaribu kufanya hivyo, Shure, nakwambia, ni Baada ya siku chache Tu, mfano wa watu wakoma watajitokeza, wataamua moja, ama kufa, ama kuishi, mtu huwezi kaa na njaa kisa eti nje kuna corona, wajaribu waone, kuna watakao kufa Kwa sababu watapigwa eiza na police ama watu watakaokuwa wakilinda watu wastoke Nje
Hili janga salama yake, ni mtu ujikabidhi Kwa Mungu, ili ukifa iwe faida