Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Trump asimamisha misaada kwa nchi nyingine kwa siku 90 ili kupitiwa upya. Tanzania nayo kuathirika

Wakuu,

Utawala mpya wa Rais wa Marekani Donald Trump umesitisha na kuzuia misaada ya kimarekani kwa nchi za kigeni.

Marco Rubio ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameripotiwa kutuma barua kwenye balozi zote duniani kusitisha miradi ya maendeleo ambayo inafadhiliwa na Marekani ndani ya siku 90.

Barua ya Marco Rubio imedokeza kuwa ndani ya siku hizo 90, uongozi mpya wa Trump utafanya uchambuzi kuhusu namna ambavyo Marekani itakuwa inatoa misaada yake kwa nchi nyingine ambapo Rais Trump alidokeza kuwa misaada yote inayotolewa nchi za nje lazima ijibu maswali matatu rahisi:
  1. Je, misaada hiyo inachangia kuifanya Marekani kuwa salama?
  2. Je, inaiimarisha Marekani kama taifa lenye nguvu?
  3. Je, inachangia ustawi wa kiuchumi wa Marekani?

Kwa hiyo ndni ya siku 90 iwapo kuna mradi wowote kutoka Marekani ambao hautajibu hayo maswali matatu muhimu kuna uwezekano mkubwa mradi huo ukafutwa kabisa


Uamuzi wa Trump utakavyoiathiri Tanzania

Kwa nchi za Kiafrika na dunia ya 3 kwa ujumla, uamuzi wa Trump ni pigo kubwa kwa taasisi na miradi ya maendeleo inayotegemea msaada kutoka Marekani.

Ukweli mchungu ni kwamba hata baada ya mapitio hayo, hakuna uhakika kuwa mambo yatarejea kama kawaida.

Hatua hiyo imeshaanza kuleta athari na kusababisha wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi wa miradi inayofadhiliwa na Marekani, wengi wao wakiwa hawana uhakika wa ajira zao.

Gazeti la Mwananchi lilipata wasaa wa kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi ambao baadhi ya miradi yao inafadhiliwa na Marekani wakieleza wasiwasi yao juu ya uamuzi huo wa Rais Trump.

Esther Jackson (sio jina lake halisi), meneja wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi jijini Dar es Salaam, amesema kuwa tangazo hilo limeathiri miradi yao moja kwa moja.

"Baada ya maagizo yale, tulitangaziwa ofisini kuwa miradi tuliyokuwa tunaitekeleza itasimama kwa muda. Kwa sasa tumeambiwa hatuna haja ya kwenda kazini mpaka pale tutakapofahamishwa vinginevyo," amesema Jackson.

================================================================

Secretary of State Marco Rubio ordered an immediate stop to the flow of almost all U.S. foreign assistance Friday pending a review, according to an internal State Department cable obtained by NBC News.

The directive sent to all consular and diplomatic posts follows President Donald Trump’s executive order Monday pausing new obligations and disbursements of foreign aid pending reviews "for programmatic efficiency and consistency" with U.S. foreign policy, within 90 days of the order.

The memo stipulates that U.S. departments, agencies and entities “shall not provide foreign assistance funded by or through the Department and USAID without the Secretary of State’s authorization or the authorization of his designee."

Source: Financial Times, Mwananchi
Nimeipenda hiii
Kwa hayo maswali hakuna watakao survive
 
Nyinyi ni vilema mpaka mtegemee misaada?
Yaani naomba ikiwezekana waikate jumla ili akili zitukae sawa.

Yaani hela za kuhudumia raia hazipo mpaka mnategemea nchi nyingine ziwasaidie,lakini hela za kununu mashangingi mapya kila mwaka na mafuta ya kuyaendesha,kununua wapinzani ili waamie ccm,kunua magoli, kutoa zawadi kwa mashehe na maasikofu, za kiiba na kwenda kuficha uswizi ,za kupeleka wasanii korea hizo zipo za kutosha.
Pumbavu kabisa.
Inashangaza sn
Trump akate kabisa hiyo misaada
 
Mkuu mataifa ya China na Russia watalitumia vizuri hilo gape, trump ni mwenda wazimu sana, Wenzake walikuwa wanazipembejea nchi duniani kwa mahusiano yeye ndio anaenda kuvunja, Trump sio mtu sahihi sana kwa uongozi wa Marekani
Ni kulikuwa na vita sana kati ya nchi za kisovieti na US kuhusu influence in africa.

Ni wakati sasa china kuwekeza zaidi na kuwa na influence africa kuliko US kama hata tumia fursa hio
 
1738040741939.jpg
Ni kweli haya madai
 
Acha kukariri unafikiri NGO zote zilikuwa zinapata FUND kutoka USAID?

Mfano Mimi nipo WFP unafikiri nategemea USAID pekee
Mjinga tu huyo kutwa wanalalamika ajira hakuna. Wanasahau kwenye haya maisha kila mtu ana take risk zake!
 
Back
Top Bottom