Trump asisitiza kuwarejesha kwao wahamiaji

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipate ushindi wake, rais mteule Donald Trump alisema "hakuna bei" kwa mipango yake ya kufukuzwa nchini. Akizungumza na NBC News jana, alisema:

Kipaumbele chake cha kwanza ni "kuimarisha ulinzi wa mpakani", na utawala wake hauna "budi" ila kutekeleza kuwarejesha makwao wahamiaji wengi - hilo tu ndio suluhisho.

Sera yake ya uhamiaji ni baadhi ya masuala yaliyomfanya kupata ushindi huo, Trump alisema, na wapiga kura walikuwa wanatafuta mgombea "atakayewasaidia" Wamarekani kwa maarifa.

Trump pia alibainisha jinsi kampeni yake ilivyovutia wapiga kura wengi zaidi katika uchaguzi huu - unaweza kusoma zaidi kuhusu hilo hapa Simu zake na Makamu wa Rais Kamala Harris na Rais Joe Biden kufuatia uchaguzi zilikuwa "za heshima sana"

Bado hajazungumza na Rais wa Urusi Putin, lakini akaongeza: "Nadhani tutazungumza" - unaweza kufuatilia kauli ya Putin kuhusu ushindi wa Trump hapa
 
Kwenye suala hili hili la Uhamiaji Trump akili-handle vibaya linaweza likamletea misukosuko kwenye Utawala wake. Awe makini na Mwangalifu Sana kushughulikia suala hili, utawala wake unaweza kuja kuwa mgumu Sana na pengine hata anaweza akaondolewa madarakani kwa njia ya Impeachment endapo kama hatakuwa mwangalifu kwenye suala hili. Kimsingi Marekani purely ni nchi ya Wahamiaji, hata yeye mwenyewe Donald Trump chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Ujerumani.
 
Wakufukuzwa wafukuzwe wale wenye itikadi kali za kidini/magaidi ya kidini na wauza mihadarati. Wahamiaji wa kiafrika na wale wengine wasio na itikadi kali kuwafukuza ni kuwaonea tu kwani wamezamia huko kutafuta maisha bora
 
Kwenye suala hili hili la Uhamiaji Trump akili-handle vibaya linaweza likamletea misukosuko kwenye Utawala wake. Awe makini na Mwangalifu Sana kushughulikia suala hili, utawala wake unaweza kuja kuwa mgumu Sana na pengine hata anaweza akaondolewa madarakani kwa njia ya Impeachment endapo kama hatakuwa mwangalifu kwenye suala hili. Kimsingi Marekani purely ni nchi ya Wahamiaji, hata yeye mwenyewe Donald Trump chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Ujerumani.
Mmatumbi unamfundisha rais wa muhula wa pili wa marekani nini cha kufanya.
 
Kuna reply moja matata sana imefutwa hapa.

Aisee imekaa kibabe sana na kama kweli yaliyomo kwenye ile reply kaongea mbabe wa nchi za kiafrika basi safi sana yaani.

Ukweli ndiyo ule, nchi zetu za kiafrika kama viongozi hawajui kulinda na kusimamia rasilimali zilizopo.

Viongozi wa kisiasa wanataka kujijazia minyama wao wenyewe.

Waafrika tunachukiana sisi kwa sisi na hatuwezi kujitawala japo tuna wasomi.

Waafrika tunaemda shule ila hata vyoo tunasubiri mmarekani aje ajenge.

Mambo ni mengi ila kazi kazi kwa ndg Trump 😂!.
 
Kwenye suala hili hili la Uhamiaji Trump akili-handle vibaya linaweza likamletea misukosuko kwenye Utawala wake. Awe makini na Mwangalifu Sana kushughulikia suala hili, utawala wake unaweza kuja kuwa mgumu Sana na pengine hata anaweza akaondolewa madarakani kwa njia ya Impeachment endapo kama hatakuwa mwangalifu kwenye suala hili. Kimsingi Marekani purely ni nchi ya Wahamiaji, hata yeye mwenyewe Donald Trump chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Ujerumani.
Kama Trump naye ni mhamiaji sijui toka Ujerumani, kwa hiyo, aachie watu waingie bila utaratibu. Mfanye ujinga, muuze rasilimali zenu, muuze nchi zenu, huko,.mfanye uhalifu kwenu huko halafu mkimbilie Marekani. Awatimue wote wajenge nchi zao au waingie kwa utaratibu.
 
Uwezi ukalinganisha Mhamiaji kama Elon na Roma mkatoliki au Mange
 
Kwenye suala hili hili la Uhamiaji Trump akili-handle vibaya linaweza likamletea misukosuko kwenye Utawala wake. Awe makini na Mwangalifu Sana kushughulikia suala hili, utawala wake unaweza kuja kuwa mgumu Sana na pengine hata anaweza akaondolewa madarakani kwa njia ya Impeachment endapo kama hatakuwa mwangalifu kwenye suala hili. Kimsingi Marekani purely ni nchi ya Wahamiaji, hata yeye mwenyewe Donald Trump chimbuko lake ni Mhamiaji kutoka nchini Ujerumani.
Huyu ni mwehu! Watamwondoa Kwa njia yoyote! Amekoswakoswa na Risasi mara mbili lakini anajimwambafai? Kennedy ilikuwaje?
 
Kuna reply moja matata sana imefutwa hapa.

Aisee imekaa kibabe sana na kama kweli yaliyomo kwenye ile reply kaongea mbabe wa nchi za kiafrika basi safi sana yaani.

Ukweli ndiyo ule, nchi zetu za kiafrika kama viongozi hawajui kulinda na kusimamia rasilimali zilizopo.

Viongozi wa kisiasa wanataka kujijazia minyama wao wenyewe.

Waafrika tunachukiana sisi kwa sisi na hatuwezi kujitawala japo tuna wasomi.

Waafrika tunaemda shule ila hata vyoo tunasubiri mmarekani aje ajenge.

Mambo ni mengi ila kazi kazi kwa ndg Trump 😂!.
Upi umuhimu wa hiyo elimu sasa?
 
Uwezi ukalinganisha Mhamiaji kama Elon na Roma mkatoliki au Mange
Bado hujatussidia. Roma amefikaje USA au mange ? Kwa nini nanyi msizalishe mabilionea watakaowekeza USA, badala yake mnazalisha wabeba mabox kwao. Nani anamtaka maskini kwake. Hitimisho. Jenga watu wako, zuia wizi wa rasilimali zako. Jenga uchumi wa nchi yako. Penda watu wako. Linda watu wako. USA haikushuka toka mwezini. Ilijengwa ililindwa hata kama utawaita wahamiaji miaka ya 1400 AD
 
Back
Top Bottom