Rais wa Marekani Donald Trump amesema mazungumzo kati ya Marekani na Iran yanatarajiwa kuanza Jumatatu baada ya kuamua kusitisha mashambulizi mapya dhidi ya Iran ili kutoa nafasi kwa diplomasia.
Trump amesema kulikuwa na mpango wa Marekani kutekeleza “shambulio kubwa zaidi tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia” dhidi ya Iran, lakini akausitisha ili kutoa fursa ya kufikiwa kwa makubaliano.
“Ni wazi hawataki kushambuliwa. Walijua ukubwa wa shambulio hilo kwa sababu waliona maandalizi yake yakifanyika,” Trump amewaambia waandishi wa habari akiwa ndani ya ndege ya Air Force One.
Soma zaidi:Iran yafika Pakistan kwa mazungumzo
“Sasa tunachofanya ni kuzungumza nao kupitia mazungumzo ya kidiplomasia. Mazungumzo hayo yanaanza kesho alasiri.”
Hajatoa maelezo kuhusu mahali yatakapofanyika wala ni nani watakaoshiriki.
Siku ya Jumamosi, Trump alikuwa ameondoa vitisho vya kushambulia Iran baada ya kusema kuwa “misingi” ya makubaliano ilikuwa tayari imewekwa.
Katika kauli zake za hivi karibuni, amesema kuwa Iran pamoja na washirika wa Marekani, ambao ni Saudi Arabia, United Arab Emirates na Qatar, wamemsihi asitishe mashambulizi hayo.
“Washirika walipoomba tusitishe, unalazimika kusema, ‘Basi tuone kitakachotokea.’ Sababu ya wao kuomba hivyo ni kwa sababu wanaamini kuna uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano,” amesema.
Aliongeza kuwa kuna makubaliano yanayohusu Strait of Hormuz, na baadaye yatafuatia makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran au kile alichokiita kuiondolea Iran uwezo wa nyuklia.
Trump pia amesema Mwanamfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, amemhimiza asiendelee na mashambulizi hayo, akionya kuhusu athari zisizotarajiwa.
“Je, nchi yao inaweza kufurika kwa wakimbizi na kusababisha maafa? Mambo mengi mabaya yanaweza kutokea,” amesema.
Diplomasia ya kikanda yaongezeka
Tangazo la Trump lilikuja saa chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, **Abbas Araghchi>, kufanya mazungumzo ya pili kwa njia ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan Al Saud, yakihudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Pakistan, Asim Munir, kujadili juhudi za hivi karibuni za kidiplomasia.
Vita vilianza Februari 28 baada ya Marekani na Israel kufanya mashambulizi ya kushtukiza dhidi ya Iran. Hata hivyo, miezi ya mazungumzo ya mara kwa mara ilileta vipindi vya utulivu.
Makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano, yaliyohusisha pia kufunguliwa tena kwa Mlango wa Hormuz, yalivunjika. Tangu wakati huo Iran imeimarisha udhibiti wake wa njia hiyo muhimu ya baharini huku mashambulizi kati ya pande hizo yakirejea katika wiki za hivi karibuni.
Bei za mafuta zashuka
Bei za mafuta zilishuka kwa kiasi kikubwa baada ya Trump kuachana na mpango wa kuanzisha operesheni mpya ya kijeshi dhidi ya Iran, hali iliyopunguza hofu ya kuvurugika zaidi kwa usafirishaji wa nishati kutoka Ghuba ya Uajemi.
Bei ya mafuta ya Brent ilishuka kwa dola 4.08, sawa na asilimia 4.64, na kufikia dola 83.85 kwa pipa.
Wakati huo huo, mafuta ya West Texas Intermediate (WTI) yalipungua kwa dola 4.01, sawa na asilimia 4.74, na kufikia dola 80.66 kwa pipa.
Kuporomoka huku kulifuta sehemu ya ongezeko la zaidi ya asilimia 20 lililorekodiwa mwezi uliopita, baada ya mapigano mapya kati ya Marekani na Iran pamoja na mashambulizi dhidi ya meli za kibiashara karibu na Oman kuongeza hofu kuhusu usalama wa usafirishaji wa mafuta kupitia eneo hilo.