Trump awajibishwa kwa kashfa ya unyanyasaji wa kingono, Kumlipa E. Jean Carroll $ 5 milioni

Nasema kule US hayo mambo ya ubakaji na kashfa yapo sana na ni jambo lilozoeleka kwa watu wengi na ukijaribu kuwapekuwa wamerekani wengi wako victimed, sasa ukija kwenye Politics au mambo mengine makubwa ya nchi watu ndio hurudi nyuma kupekuwa pekuwa ili kumtia mtu hatinai kwa lengo la ku-take advantage iwe kisiasa au vyenginevyo.

Trump alipoonekana huenda akawa ni mwiba na anaushawishi wa kutaka kurudi madarakani ndio wameenda kufukua hayo makaburi ili aje azuiwe na hiyo sheria watu wa-take advantage waendelee na malengo yao. iko hivyo ndugu.

Ndio maana Mahakama imemuhukumu Trump amlipe yule mwanamke $ milioni 5 tu hela ambayo kwa trump ni kama maji ya kunywa tu kutokana na utajiri wake., lakini hapo hili jambo litaenda kumuathiri kisiasa ambapo ndio kiini cha malengo.

Lakini sasa huko kwenu ni tofauti mtu anaweza pewa kesi tu ambayo haipo wala kuwahi kutokea
 
Haya yanayomkuta Trump yakiwakuta wapinzani wa nchi zetu huku Africa utasikia watu walewale wanaosifia Trump kuhenyeshwa ndio wanakosoa wakisema mpinzani anaonewa.

Kweli dunia bila unafiki mambo mengi hayatasonga mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…