Asante kwa uzi,hizo siasa za ubaguzi na kuitenga Marekani na jumuia za kimataifa ndiyo zilizompa uraisi Trump kwenye ule uchaguzi aliopita,halafu hiyo point ya mwisho hapo uliyoielezea kuhusu udhaifu wa raisi mwanamke kwenye siasa za dunia ambazo kwa sasa zimegubikwa na vita na migogoro mikubwa isioisha,zilimuangusha pia Hilary Clinton na Trump akapeta,Marekani bado haipo tayari kutawaliwa na raisi mwanamke,Kuna undi kubwa la wapiga kura ambao wana hiyo mentality ya kutaka Marekani iendelee kuwa mbabe duniani wanahitaji Kiongizi kama Trump,kwa Mimi binafsi na uzoefu wangu wa kufuatilia chaguzi mbalimbali duniani,namuona Trump akirejea madarakani na Chama chake cha Republican,japo hayo siyo matarajio ya watu waliowengi duniani.