POTOSHI Trump: Iran walipiga meli yetu tukaikimbiza tuogopa tusije kufa

POTOSHI Trump: Iran walipiga meli yetu tukaikimbiza tuogopa tusije kufa

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wanaukumbi.

Trump: "Iran ilipiga shehena kubwa zaidi ya ndege duniani kutoka pande 17 tulikinbia ili kuokoa maisha yetu ilikuwa tumekwisha"

Tulikuambia ilipigwa na ikakimbia.

Sasa Trump anathibitisha.

Screenshot 2026-03-30 105503.png
 
Tunachokijua
Kuanzia Machi 28, kumekuwa na na kipande cha video ikimuonesha Rais Donald Trump akizungumza na kuambatanishwa na ujumbe unaosomeka:

Breaking — Trump: “Iran hit world's biggest aircraft carrier from 17 angles we ran for our lives it was over”We told you it was struck and it ran away. Now Trump is confirming it. Tazama hapa

Ikiwa na maana kuwa:

Habari za hivi punde - Trump: “Iran ilishambulia meli kubwa zaidi ya kivita duniani kutoka pande 17, tulikimbia kuokoa maisha yetu, ilikuwa imekwisha.”

Uhalisia wa madai hayo ni upi?

Ufuatiliaji kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hiyo ni halisi lakini imehaririwa kwa kuondolewa baadhi ya sehemu ili kupotosha uhalisia.

Video nzima ikiwa na urefu wa saa 1:18:26 ilichapishwa katika ukurasa rasmi wa ikulu ya Marekani (White House) ikiwa na kichwa cha taarifa kinachosemeka: "President Trump Delivers Remarks at the Future Investiment Initiative".

Rais Trump alikuwa akitoa hotuba katika jukwaa la Future Investiment Initiative, ambapo tukio hilo lilifanyika Machi 27, huko Miami, Florida nchini Marekani.

Katika hotuba yake Trump aliyatamka maneno ya meli ya kivita kushambuliwa kutoka katika pande 17 lakini hakuwa anaizungumzia Iran na badala yake alikuwa akizungumzia tukio la kukamatwa kwa Rais Maduro na waliokimbia walikuwa ni wanajeshi wa Venezuela.
Back
Top Bottom