Trump kuiondoa Marekani kwenye Muungano wa NATO

Trump kuiondoa Marekani kwenye Muungano wa NATO

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anafikiria kwa kina kuiondoa Marekani kutoka kwa Muungano wa NATO baada ya washirika wa muungano huo kushindwa kuunga mkono hatua ya kijeshi za Marekani dhidi ya Iran, kulingana na mahojiano na gazeti la Uingereza, Daily Telegraph.

Soma pia Marekani azidiwa na Iran, aomba msaada NATO lakini amekataliwa

Trump aliuelezea Muungano huo kuwa “dhaifu ya kuonekana kuwa na nguvu."

Alisema kuiondoa Marekani kutoka katika mkataba huo wa ulinzi sasa “hakuhitaji tena kufikiria upya,” gazeti hilo liliendelea kuripoti, na kuongeza kuwa, kwa muda mrefu amekuwa na mashaka kuhusu uaminifu wa NATO.

“Sikuwahi kushawishika na NATO. Siku zote nilijua walikuwa dhaifu japo wanaonekana kuwa na nguvu, na Putin anajua hilo pia, kwa kweli.”

1775044149078.png

=============

U.S. President Donald Trump said he was strongly considering pulling the United States out of NATO after allies failed to back U.S. military action against Iran, according to an interview with Britain’s Daily Telegraph.

Trump described the alliance as a “paper tiger” and said removing the United States from the defence pact was now “beyond reconsideration,” the newspaper reported. He said he had long held doubts about NATO’s credibility.

“Oh yes, I would say [it’s] beyond reconsideration,” Trump told the newspaper when asked about whether he would reconsider U.S. membership of the alliance after the conflict.

“I was never swayed by NATO. I always knew they were a paper tiger, and Putin knows that too, by the way.”

Source: CTV News
 
Sababu nyingine hii Stamer anataka kufanya kikao na nchi zinazo potisha mafuta Hormuz. So naona wameamua kuchagua diplomasia badala ya ujinga wa kusupport vita isiyo na maana na faida kwao.
 
Putina anatamani Trump atangaze hata Sasa hivi USA kujitoa NATO.
Maana NATO ndio pasua kichwa kwake wala sio EU.
Mfadhili mku akijitoa kinabaki chama kama CUF ya Lipumba without Maalim. Kitu watu wengi hawaelewi kwamba Trump lengo lake kuu ni kuuonyesha ulimwengu wapi panavuja na wapi pamezibwa vizuri. Tutaziona kila rangi..

Alianza WHO, Venezuela chali, Iran ndio ntolee hivyo mbele ya Macho na China na Russia, Ulaya wakitazama... Baadae kiduku na China wakilinzisha huko far east Japan na south Korea kama hawajaonyesha ushirika kwa kaka mkubwa wasianze kulia lia.

pUTIN nae anasuburi tu kipyenga kipulizwe USA kama Ukreni vita haijaisha.
 
Aitoe tu Marekani kwenye muungano wa NATO. Anamtishia nani?

Anadhani UE inaitegemea kivile marekani kumbe la hasha. Kwanza mataifa ya ulaya yamepitia mambo mengi sana tangu Dunia kuumbwa.

Nyambafu sana huyu Mzee mwenye ugonjwa mkali wa akili.
 
Trump akijiondoa NATO anajiweka kwenye hatari ya kushindwa kupenyeza ushawishi nchi za ulaya zinapofanya biashara na mahasimu wake wa kibiashara mfano China. Umoja wa NATO ni kete yake muhimu sana ya ushawishi hata kwenye mambo nje ya masuala ya jeshi na vita.

Hii sera ya Trump ya kuitenga USA na dunia kwa uchambuzi wangu wa level ya mtanganyika aliyeshiba mihogo naona anakosea. Unless mifumo ya dunia inahama na sisi wasindikizaji hatujui kinachoendelea.

Otherwise, kama mambo yapo vile vile nguvu ya USA ipo kwenye ushawishi wake, akipoteza ushawishi anakua kubwa jinga.
 
Anapiga domo Tu huyo, nchi za ulaya ni muhimu Sana kwenye mambo ya usalama ya Marekani...Trump anafanya baadhi ya vitu kihuni huni, na Hali hii inazidi kuleta wasiwasi wa kuaminiani, US anaingia vitani kwaajili ya Israel na huu ni mtego Kwa nchi za ulaya, hii vita kama zilivyo nyingine za hapo nyuma ni Israel ndo anawashawishi...

Halafu suala la urais ni Jambo la kupita, Leo hii unatishwa na Trump Kesho ataingia mwingine na inawezekana mkaonekana wapumbavu wa mwisho Kipindi trump anakula zake pension Yake ya kustaafu.
 
Trump sio MTU wa kumuamini hata kidogo huyu Mzee anaikoroga hii vita Kwa maneno na vitendo... kwenye vita hii propaganda imekuwa silaha muhimu Sana Kwa kila upande
Alikulia New York kwenye mazingira ya mabully Mafia, na akachukua tabia hizo za bully, za kutisha tisha na kutoa matusi hovyo hovyo. Uanachama wa NATO ni treaty iliiyoidhinishwa na Bunge. Hawezi kujiioa NATO kienyeji enyeji tu bila idhini ya Bunge. na Mwaka 2023 Bunge liliongeza ugumu wa kujitoa kwa kutaka maseneta zaidi ya 60 kati ya 100 wakubali kujitoa. Halafu baada ya hapo kuna transition ya zaidi ya mwaka mzima kukamilisha mchakato. Muda huo Trumpo hatakuwa madarakani.

Kwa hiyo hapo anachofanya ni ile tabia iliyojengwa kichwani mwaka ya vitisho, na matusi kama ilivyo kwa bully yeyote lakini hawezi kujitoa.
 
Huyu nae apunguze kelele ile janja ya kutaka nchi za watu waingie kukusandia then wewe hujiondoe kwenye masala wenzio NATO wameistukia USA inaitaji NATO kuliko NATO inavyoitaji USA ajitoe apiunguze kelele
 
Bado ajasema tumpe mda 👇👇
 

Attachments

  • 1774978362327.jpg
    1774978362327.jpg
    111.9 KB · Views: 30
Back
Top Bottom