econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kituo Cha televisheni Cha ABC kimeamua kukubali kumlipa Rais Donald Trump kiasi Cha Bilioni 37 za kitanzania kama fidia ya kumchafulia jina Rais huyo mteule wa Marekani. Rais mteule Donald Trump aliamua kufungua kesi dhidi ya ABC baada ya mtangazaji wa ABC Bwana George Stephaphoulous kutangaza ya kwamba Trump ni mbakaji na kwamba alipatikana na hatia ya kumbaka mwanamke.
Ukweli ni kwamba mahakama haikusema hivyo kwamba Trump alikuwa na hatia ya kubaka bali alipatikana na hatia ya shambulio la aibu dhidi ya mwanamke huyo na sio ubakaji. Trump alienda mahakamani kudai fidia ya kuchafuliwa jina kwa kuitwa mbakaji. Baada ya kuona Trump kafungua kesi, ndipo ABC walipoamua kuomba msamaha na kukubali kesi iishe nje ya mahakama na kukubali kumlipa Trump kiasi Cha Dollar milioni 16 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 38 za kitanzania.
Source: CNN