Trump kuzindua mtandao wa kijamii wa TRUTH Social

Trump kuzindua mtandao wa kijamii wa TRUTH Social

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ametangaza mipango ya kuzindua mtandao mpya wa kijamii, uitwao TRUTH Social.

Amesema jukwaa hilo "litakabiliana na jeuri ya kampuni kubwa za teknolojia ", akizishutumu kwa kunyamazisha sauti za wapinzani huko Marekani.

Kampuni ya Trump Media & Technology Group (TMTG), ambayo yeye ni mwenyekiti wake, pia inakusudia kuzindua huduma ya usajili wa mahitaji ya video.

Bw. Trump alipigwa maarufuku katika mitandao ya kijamii au kufungiwa na mitandao kama ya Twitter na Facebook baada ya kundi la wafuasi wake kuvamia Bunge la Marekani Januari mwaka huu.

Yeye na washauri wake tangu wakati huo walidokeza kuwa wanapanga kuunda mtandao hasimu wa kijamii.

Toleo la mapema la biashara yake ya hivi karibuni, TRUTH Social, itakuwa wazi kwa wageni waalikwa mwezi ujao, na kutakuwa na "uzinduzi wa kitaifa" ndani ya miezi mitatu ya kwanza ya 2022, kulingana na taarifa ya TMTG.

"Tunaishi katika ulimwengu ambao Taliban ina uwepo mkubwa kwenye Twitter, lakini Rais wako mpendwa wa Marekani amenyamazishwa," aliandika Bw Trump.

Mapema mwaka huu, alizindua Kutoka kwa Dawati la Donald J Trump, ambayo mara nyingi ilikuwa ikiitwa blogu.

"Kila mtu ananiuliza kwa nini mtu asisimame kupinga makampuni makubwa ya teknolojia? Sawa, tutafanya hivyo hivi karibuni!" aliongeza.
 
Rais wa wa muhula uliopita wa Marekani Donald Trump ametangaza rasmi kuwa hivi karibuni atazindua Mtandao wake wa Kijamii ambao utaitwa "TRUTH"

Maamuzi haya amefanya kufuatia kufungiwa kutumia Facebook na Twitter baada ya kudaikwamba, Media, Tech Giants na Democrats walimfanyia figisu kuaminisha umma kwamba alichochea vurugu katika Majengo ya Bunge Marekani January 6 2021.

Kwa upande wangu Trump alikuwa raisi bora mno, Ila kwa kuwa wengi kwenye hili jukwaa ni watu wa kuhitimisha vitu kwa taarifa za Far Left Main stream Media kama CNN, MSNBC, n.k sitashangaa comment za kumponda Gwiji huyu
 
Wala sishangai, maana wabongo wengi ni wapenzi wa CNN wataalamu wakubwa wa kupika habari.

Hta mauaji ya George Floyd yaliyochochea Black Lives Matter ni upuuzi tu, Huyo George floyd alikuwa jangiri kubwa sana
😄😄😄 Trump tower.
 
Ndio alistahili kufa vile jmn?.
Tuthamini maisha ya watu wengine
Mtu alikamatwa ananunua bidhaa kwa pesa feki, muuza duka kawapigia simu mapolisi waje kumkamata, polisi wamefika hapo wanataka kumuweka chini ya ulinzi, jamaa hataki kutoa ushirikiano, kila wakimwingiza anatumia nguvu kutoka, na muda huo alikuwa amaelewa madawa ya kulevya (usitumie google tumia duckduckgo alafu search "george floyd baggie) utaona sehemu ya video iliyokamatwa kuna kimfuko cha unga wa madawa kilidondoka wakati anakamatwa.

Licha ya hivyo huyu Floyd ni muhalifu sana, gerezani kaingia na kutoka kama sebuleni, aliwahi vamia nyumba akamuta mmama mjamzito, akamnyooshea bunduki kwenye tumbo lake atoe pesa lasivyo ana shoot.

Kiufupi huyu bwana alikufa kwa kulewa sana madawa na kutokutoa ushirikiano.

Tafuta video nzima yenye zaidi ya saa uone kila kitu, sio ile imekatwa katwa.

Maskini ya Mungu huku Bongo ndio kabisaaa!! watu wanacheki cnn ndio wakawa brain washed kama watoto
 
Trump wamarekani wqnamkubali sana , asingekufa george floyd jamaa angeshinda tena
 
daah we jamaa
unajiandikia tuu
 
Back
Top Bottom