Trump: Nchi za BRICS zenye mpango wa kuikwepa Dola ya Marekani zitakumbana na ushuru wa asilimia 100, Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine

Vita ya biashara inakuja...
 
Ukipandisha ushuru watakao umia ni watumiaji wa mwisho wa nchini kwako.

Kafuatilie trade war ya marekani na China 2018 Trump hajaanza kuwa mwendawazimu leo.

Uzuri ana deal na mataifa yenye akili yanayo nufahika na upumbavu wake.
Umesema vyema

Tariffs ni hidden tax itakayolipwa na Wamarekani na sio Wachina. Hiyo tariffs ni pigo kwa Wamarekani

Pili, itawaongezea production cost manufacturers wa Marekani wanaotegemea kuimport bidhaa China ili wafanye uzalishaji mwisho wa siku tena atakayebeba huo mzigo ni final consumer aliyeko Marekani

Trump atalazalisha inflation tu
 
Trumpet anaweza akawa akili kubwa ila wewe ukawa akili ndogo sana unadhani brics imeanza kuanzishwa Jana na leo na marekani hawakujua kama inatishia uwepo wao kwanini wasinge hamishia hayo makampuni yao tokea awali trumpet unadhani hakuwahi kua rahisi wa marekani kabla kwanini hajafanya haya uloyasema kabla kijana unaelewa maana ya uchumi hata kwa asilimia moja kama kila mtu angekua anatumia kile anacho kizalisha kwakua tu anaweza basi uchumi usingekua na maana ngoja nikutoe tongo tongo kidogo hata uwe unatengeneza mpaka miti ila lazima uuze ama ununue ndani na nje ndio utapata maana na dhana halisi ya uchumi na kama kwa kutegemea tu soko la ndani basi uchina ana nafasi ya juu kuipiku marekani sababu kuu mbili nakupa ambazo marekani hana na hautakua nazo moja population ya china kubwa mbili skilled workers someni vijana nyie ndio mnatufanya waafrika wote tunaonekana vilaza
 
Exactly na matokeo yake products za China zitakua expensive kuliko za ndani au nchi zingine, so wanunuzi watanunua za wapi?? Common sense tu wala sio majazba, imani au uchawi - typical business
 
Huyo Marekani yeye anauza wapi? Ukitoa ulaya ambayo kwanza uchumi wao usha fikia kikomo cha kukua, Marekani anategemea kuuza China ,India na Brazili.

Pia kumbukeni Bricks wana natural resources za kutosha hasa China Russia,Irani, Brazili.
Tatizo moja unafiki.. china hachelew kwenda kuongea na sim chooni na USA
 
Tangu 2018 Trump ameanza kupambana na China kwenye trade war, sanctions, tariffs, decoupling na derisking

Hakuna hata kimoja alichofanikiwa nashangaa wanaozisifu hizo ngonjera zake.

Wachina walishampuuza kitambo
 
Mchina ndumilakuwili atawachomolea fyuzi wenzake.....
China ni gaidi wa uchumi,yeye kazi yake ni kukusanya tuu hakuna jingine.Hawajui hata kuchangia maafa wao ni kukusanya na kuuza tuu,kwanini Hawa watu Wana roho mbaya hivi,ilikuwaje wakakua hivi na huku Japan ikipotea kiasi hiki,India nao ni walewale wanajua kukamua tuu
 
Ukiweka mahaba na chuki pembeni na ukautazama uchumi wa dunia ulivyo na namna biashara za dunia zinavyoendeshwa ni wazi kuwa mataifa itawachukuwa miaka mingi ya damu, tabu, na mateso kuachana moja kwa moja na Dola ya Marekani......

Kwa namna Marekani ameisuka nchi yake, uchumi wake na mifumo yake ya kibiashara na siasa zake ni wazi kuwa kila nchi inatamani kuuza au kushirikiana kiuchumi na Mmarekani...

Wafanyabiashara, matajiri na wawekezaji karibia wote kutoka pande zote dunia wanajiona wapo salama wakiwekeza Marekani kuliko nchi nyingine yoyote..........

Kwa kifupi anguko la Dola lipo lakini mizizi ya dola imeenda mbali na itachukuwa miaka mingi sana kuitoa.......

Je mataifa yapo tayari kuziingiza kwenye dhiki nchi na wananchi wake kwenye kupambana na anguko la Dola......je dunia ipo tayari kuzikabili athali za anguko la dollar ya Marekani na imejiandaaje kwa muda huo hadi kupata nyingine itakayokuwa stable kama Dola....???

Lisemwalo lipo....
 
Wakulima wakimarekani walilalamika sana upuuzi wa DT 2018 China walipojibu mapigo

Uzuri huyu kichaa Trump yeye huwa anaanza alafu wenzake wanajua namna ya kumaliza
 
Rubbish,
Umeanza kwa kujihami eti ukiweka mahaba pembeni, halafu ukayatumia hayo hayo mahaba!

Wewe mmarekani mweusi wa Nzega unafikiri unaweza kusema jambo baya dhidi ya Marekani?
Wagalatia mmekariri sana.
 
Wala usijali bwana utamu, dollar haitaanguka kwa uchawi na maombi, take or leave it
Uzuri anguko la dollars wala haihitajii uwe na elimu kuubwa kuliona kama linazidi kuendelea marekani kama empire inaanza kumeguka taratibu kwasasa inaanza ushawishi lengo kuu hapa dollars imeporomoke na ndio inaendelea hakuna anae omba dua watu wanakaa chini wanafanya majambo kaa hapo hapo
 
Hapo ambaye hajui mlango wa ziada wa kutokea ni huyo babu anaye tizamana na PUTIN lkn wengine hasa PUTIN mwenyewe akiingia chakani unakuta alishajua kabisa mlango mwingine wa kutokea endapo alioingilia ukizibwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…