Trump: Nchi za BRICS zenye mpango wa kuikwepa Dola ya Marekani zitakumbana na ushuru wa asilimia 100, Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine

Trump: Nchi za BRICS zenye mpango wa kuikwepa Dola ya Marekani zitakumbana na ushuru wa asilimia 100, Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine

Kaka bila Marekani hamna China, 90% ya mapato ya China yanatoka US na anajua hilo! So ni muda wa kujitenga nao, ukipigwa 100% tariff ni kwamba hamna bidhaa yake itauzika tena US na Jinping hatokubali hili kwa namna yoyote.

BRICS ilichokosea ni kwamba imekaa ili kuua dollar sio kwa maendeleo yake, yani ni kikao cha wachawi! Ukianza vikao vya kuua wengine ni kwamba umefeli at the 1st place, maana unayetaka kumuua hatakaa kukusubiri ufanye yako bila kujilinda kwa nguvu kubwa kuliko yako! Sasa Marekani kashikilia mpini unamuuaje?
Huna akili hizo asilimia 90 za China kuitegemea Marekani imeitoa wapi ?
Unajua inauza bidhaa kiasi gani hapa duniani mpaka useme eti China anategemea Marekani kwa %90?
 
Huna akili hizo asilimia 90 za China kuitegemea Marekani imeitoa wapi ?
Unajua inauza bidhaa kiasi gani hapa duniani mpaka useme eti China anategemea Marekani kwa %90?
Sasa name calling ya nini? Ukue kijana acha uharo! Umekosa hoja? Ndio maana mnafeli
 
Tunasema kila siku dollar imeumbwa na kujengwa kwa nguvu na fitna na ubabe, na hamna wa kuishusha bila kuadhirika yeye! Mchina hawezi kwa namna yoyote kupoteza soko la Marekani! Na hamna US haitokubali kwa namna yoyote kupoteza ukaka mkubwa! Ilijaribu Euro ikafa kifo cha kawaida sembuse hizi nchi zenye umri usiozidi miaka 100? Yetu macho, wahafidhina wa Urusi na washabiki wa vita povu ruksa.
Unadhani Roman empire ottoman empire na past empire nyengine zilikua zimeuchoka ukaka mkubwa endelea kukaa hapo hapo
 
Kaka bila Marekani hamna China, zaidi ya $700+ Billion ya mapato ya China yanatoka US na anajua hilo! So ni muda wa kujitenga nao, ukipigwa 100% tariff ni kwamba hamna bidhaa yake itauzika tena US na Jinping hatokubali hili kwa namna yoyote.

BRICS ilichokosea ni kwamba imekaa ili kuua dollar sio kwa maendeleo yake, yani ni kikao cha wachawi! Ukianza vikao vya kuua wengine ni kwamba umefeli at the 1st place, maana unayetaka kumuua hatakaa kukusubiri ufanye yako bila kujilinda kwa nguvu kubwa kuliko yako! Sasa Marekani kashikilia mpini unamuuaje?
Kama ni hivyo basi China atachagua bega 😂
 
Hujui màana ya kupandisha ushur mkuu, maana yake bidhaa za ndani zitapewa kipaumbele na kuangalia soko nafuu zaidi. Kumbuka bidhaa anazozalisha china kupeleka Marekani siyo kwamba Marekani hazipo ndiyo maana umeambiwa na Mr Trump 'wonderful economy ' Sasa unahisi wamarekani Wana njaa? Kwa ufupi ni kwamba iwapo US itapandisha Kodi kwa bidhaa za china itabidi makampuni ya wamarekani yenye viwanda china kwa sababu ya cheap labours yatabidi yawe reallocated US ili kujiendesha kwa faida. Na hii itapelekea china kuanguka kiuchumi kwa raia wake kukosa ajira na serikali kukosa mapato ya mauzo. Trump akili kubwa yule Mzee.
Kwani mpaka wanakuja kuagiza hizo bidhaa kwenye nchi zingine hizo bidhaa za ndani hazikuwepo au walikuwa hawazioni?
Viwanda vya nchini Marekani vina jiendesha kwa gharama kubwa sana hivyo kufanya bidhaa zao kuwa juu pia, ndio maana raia wa Marekani wanakimbilia kununua bidhaa za nchi nyingine.
Ni sawa na sisi hapa sukari ya kiwango cha juu kutoka Brazil ina uzwa kwa 1800 wakati sukari isiyo kuwa na ubora kutoka mtibwa inauzwa 3500 hicho ndo kitakacho wakuta wamarekani.
 
Nyinyi wamarekani wa Namanga simlikuwa mna sema BRICS hamna kitu haina madhara kwa Marekani ?
Sasa iweje uanze kushindana na kitu kusicho na madhara kwako?

Nchi zilizoko kwenye brics zina miliki zaidi ya theruthi moja ya uchumi wa dunia , zinamiliki zaidi ya %60 ya population ya dunia.

Akipandisha ushuri hata maisha ya wamarekani yatakuwa magumu sana maana mfumko wa bei utakuwa mkubwa sana kitu moja wapo kilicho sababishwa chama cha Democratic kuanguka kwenye uchaguzi.
Umeiba koment yangu kijana nilikua nataka niwaulize wamarekani wa jf hapa walisema brics sio threat kwa marekani na dola yao sasa inakuaje wana haha haha namna hii hawa mabwana halaf dt ni debe tupu tuuuu
 
Sasa hiyo $750 billion ndiyo 90% ya mapato ya China katika exportation hivi una akili kweli?

Na hiyo ilikuwa ni mwaka 2022 kufikia kwaka 2023 soko la Marekani linachangia $500 billion tu kwa China

Soko la Marekani ni sawa na 2% tu ya GDP ya China na 15% tu ya total exports ya China worldwide

Kwa hiyo Trump na Marekani hawana cha kumbabaisha China.

Mchina ana masoko mengi mfano hivi karibuni soko la mataifa ya global south limekua sana linachangia 43% ya total exports za China

Na huko kwenye global south countries KWANZA Mchina amewekeza, PILI viwanda vingi katika mataifa hayo bado vina-import components, parts kutoka China ili watengeneze bidhaa za kuexport Marekani.

Mfano ni Vietnam na Mexico zinapo-export kwenda Marekani, bidhaa za Mchina zinakuwa zinaingia Marekani kupitia mataifa hayo kama 3rd party

Soma hii ripoti ya serikali ya Marekani ya Federal Reserve.

Halafu uje uniambie kati ya Marekani na China nani anamhitaji zaidi mwenzake. Msipende kuongea kishabiki.

Sehemu ya ripoti ilisema hivi:

The most important U.S. suppliers increased their own reliance on Chinese goods

In the remainder of the note, we document that the increase in China's share of U.S. suppliers' imports reflect two factors. First, the most important U.S. suppliers have increased their own reliance on Chinese imports. Second, the U.S. has imported more from countries that have stronger trade ties with China. Later, we also show evidence suggesting that rerouting of Chinese goods toward the U.S. through other countries was quite limited.
Ila isome yote uongeze uelewa ujionee Marekani hawezi kumkimbia Mchina, link iko chini hapo.

Achana na maneno ya wanasiasa angalia uhalisia wa uchumi wa Marekani unavyotegemea China

Umeambiwa us ndiyo taifa lenye uchumi mkubwa Dunia kuanzia wafanyakazi wa ndani, mpaka wale wa mashambani wanamzidi mshahara mkuu wa wilaya ya malinyi hapa nchini kwako. Bora kuwa mfanyakazi wa shambani US kuliko kuwa doctor Tanzania..
Kumbe hata hakuna unacho jua kuhusu uchumi ila unaongea kwa kunukuu sitori za vijiweni?
 
Kaka bila Marekani hamna China, zaidi ya $700+ Billion ya mapato ya China yanatoka US na anajua hilo! So ni muda wa kujitenga nao, ukipigwa 100% tariff ni kwamba hamna bidhaa yake itauzika tena US na Jinping hatokubali hili kwa namna yoyote.

BRICS ilichokosea ni kwamba imekaa ili kuua dollar sio kwa maendeleo yake, yani ni kikao cha wachawi! Ukianza vikao vya kuua wengine ni kwamba umefeli at the 1st place, maana unayetaka kumuua hatakaa kukusubiri ufanye yako bila kujilinda kwa nguvu kubwa kuliko yako! Sasa Marekani kashikilia mpini unamuuaje?
Kwamba wakati China inapata hizo dola kutoka marekani wao marekani hawapati lolote kwanza unaelewa maana ya biashara kijana au umeandika tuuu unakumbuka Huawei ilitwangwa vikwazo kila kona na tarrif kibao marekani ikiamini itakua ndio mwisho wa Huawei matokeo yake
 
Ila huyo mwendawazimu DT anaweweseka na huo umoja wa wanywa kahawa ?

Humu ifike muda vipimo vya umri vianze
Umri unasaidia nini sasa. Hao brics wanafanya biashara na Marekani pia hawawezi kuikimbia dola. Kama ingekua rahisi hivyo wangeshafanya wanachokitaka. Narudia tena ni kijiwe cha kahawa 🤣🤣🤣🤣.
 
View attachment 3166300

BRICS = Brazi, Russia, India, China, South Africa

Kaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter

Wazo kwamba nchi za BRICS zinajaribu kuachana na Dola ya Marekani huku tumekaa na kuwatazama LIMEKWISHA! Tunahitaji ahadi kutoka kwa nchi hizi kwamba hawataunda Sarafu mpya ya BRICS, wala kuunga mkono sarafu nyingine yoyote kuchukua nafasi Dola ya Marekani yenye nguvu duniani, vinginevyo zitakumbana na ushuru wa asilimia 100 kwenye bidhaa wanazoingiza na zijiandae kuaga kuuza kwenye uchumi ulionona wa Marekani. Wanaweza kwenda kutafuta “mjinga” mwingine! BRICS haiwezi kuchukua nafasi ya Dola ya Marekani katika Biashara ya Kimataifa, na nchi yoyote itakayojaribu inapaswa kuaga Marekani !

The idea that the BRICS Countries are trying to move away from the Dollar while we stand by and watch is OVER. We require a commitment from these Countries that they will neither create a new BRICS Currency, nor back any other Currency to replace the mighty U.S. Dollar or, they will face 100% Tariffs, and should expect to say goodbye to selling into the wonderful U.S. Economy. They can go find another “sucker!” There is no chance that the BRICS will replace the U.S. Dollar in International Trade, and any Country that tries should wave goodbye to America.​
In the long run huu ushuru na sanctions zitafail...
Mfano suala la kuiwekea vikwazo na kuipiga ushuru china bado halijaleta matokeo waliyoyatarajia. Makampuni ya magari ya ulaya kama VW na Benz wana hofu kama china itafanya hivyo hivyo watakula hasara zaidi.
 
Tunasema kila siku dollar imeumbwa na kujengwa kwa nguvu na fitna na ubabe, na hamna wa kuishusha bila kuadhirika yeye! Mchina hawezi kwa namna yoyote kupoteza soko la Marekani! Na hamna US haitokubali kwa namna yoyote kupoteza ukaka mkubwa! Ilijaribu Euro ikafa kifo cha kawaida sembuse hizi nchi zenye umri usiozidi miaka 100? Yetu macho, wahafidhina wa Urusi na washabiki wa vita povu ruksa.
Hakuna atakachofanya . Urusi kwa sasa anawapelekea moto huko huko NATO na USA
 
Back
Top Bottom